NI laana! Baadhi ya mastaa wamenaswa laivu wakifanya vitendo
vilivyotafsiriwa kuwa vya kifuska, Ijumaa Wikienda lina mkanda kamili.
Baadhi ya mastaa wakionyeshana ufundi wa kucheza.
Tukio hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo maeneo ya
Victoria, Dar wikiendi iliyopita ambapo kulikuwa na Kibao Kata cha mtoto
wa mjini, Rose Alphonce Nungu ‘Muna Love’.
Likishuhudia tukio hilo, Ijumaa Wikienda ambalo lilijipenyeza ndani
ya nyumba, lilifuatilia kila aina ya tukio huku likifikisha ripoti kwa
mkuu wake ambaye alikuwa ofisini akipokea matukio ya Live Dijitali.
...Burudani baada ya kukolea, hali ilikuwa hivi.
Ndani ya ukumbi huo lilishuhudia laana za aina yake ambazo zilikuwa
zikiongozwa na mwenye shughuli ambaye alikuwa akikata mauno ya ajabu kwa
staili ya ‘baba na mama’ chumbani.
Husna Maulid akionyesha ufundi.
“Duh! Yaani utafikiri watu hawajui kuwa hii
ni Kwaresma, ni full laana hebu angalia Husna Maulid, Sajent (Husna
Idd) na Davina (Halima Yahya) wakiongozwa na Muna wanavyojichetua hadi
‘makufuli’ yanaonekana,” alisema mwanadada mmoja.
Husna Idd 'Sajent' naye akionyesha machejo yake.
Katika hatua nyingine, mwanaume tata
anayejulikana kwa jina la Agrey alivua nguo na kubaki na ‘kufuli’ kisha
alipanda juu ya kiti na kuanza kuonesha staili mbalimbali za ukataji wa
mauno.
“Tobaa… jamani mwangalieni Agrey, kavua nguo anamwaga radhi…hahahaaa,” alisikika msanii mmoja wa Kundi la Vituko Show.
...Sajent na Husna wakizidi kujiachia.
Kingine kilichojiri ni pale shindano lisilokuwa rasmi la kuzungusha
nyonga lilipoibuka kati ya watoto wa Ilala linaloongozwa na Baby Tunu na
Baby Tau ambao walishindana na watoto wa Kinondoni, Sajenti na wenzake,
hali iliyosababisha watu kushindwa kuvumilia na kuinuka vitini.
Ili kunusuru hali, mshereheshaji wa shughuli hiyo, Chumi Suleiman ‘Bi
Hindu’ alilazimika kuzima muziki kuepusha laana iliyokuwa inazidi
kuvuka mipaka.
“Jamani
hata mimi nina watoto wa kiume na kike, sasa hii hali siwezi
kuivumilia, nazima muziki na shughuli ndiyo imemalizika maana wote humu
ndani tutaonekana siyo,” alisema Bi Hindu ambapo baada ya kusema tu,
aliambulia mvua ya matusi.
-Ijumaa