| 
Nay | 
Hit maker wa Muziki gani na Salam Zao Nay Wamitego ameiambia MJ FM ARUSHA kuwa anapata vitisho vingi sana kupitia wimbo wake wa Salam zao.
Akiongea na Dj Haazu
 kwenye Kipindi cha DUNDO Nay amesema mara kwa mara amekuwa akitoa 
nyimbo zake anapokea vitisho vikalai sana kwa sababu ya style ya Muziki 
wake ambao anaufanya mziki ambao amesema sio Mziki wa Diss wala Uchokozi
 bali ni Ukweli anaoungea kwenye Ngoma zake kitu ambacho wengi 
wanakichukulia kama Diss au Uchokozi wa Kimaksudi.
Ney 
amesema kupitia wimbo wa Salam zao amepata Vitisho vingi sana vya 
kuuwawa hadi kufikia hatua ya kuingiwa na woga sasa kwani wengi 
wanamtishia kumuua na wengine wakimtishia kumpoteza kimziki
 

 
