Mrisho Ngassa akishangilia baada ya Said Morad kuisawazishia Stars,
Na Mahmoud Zubeiry, Machakos
TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars imeanza taratibu
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge
baada ya kutoa sare ya 1-1 na mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia au
Chipolopolo kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos, Kenya.
Katika mchezo
huo wa Kundi B, Zambia ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ronald
Kampamba dakika ya 41, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Felix Katongo.
Zambia
walitawala zaidi mchezo huo kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi zaidi ya
nne za kufunga, lakini sifa zimuendee kipa Ivon Philip Mapunda aliyeokoa
michomo kadhaa ya hatari.
Kipindi cha
pili, Stars ilibadilika mno kiuchezaji, japokuwa wachezaji waliomaliza kipindi
cha kwanza ndiyo wote waliorejea kuanza ngwe hiyo ya lala salama.
Kutokana na
mshambulizi mfululizo langoni mwa Zambia, Bara walipata kona dakika ya 48
ambayo ilikwenda kuchongwa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na kuunganishwa nyavuni
na Said Morad kwa kichwa.
Baada ya bao
hilo, Zambia walianza kuutafuta mpira kwa tochi na kama si umahiri wa kipa wao,
Nsabata Toaster kuokoa hatari nyingi, Stars wangeweza kuondoka na
ushindi.
Kwa matokeo
hayo, Burundi inaongoza kundi hilo baada ya kuifunga Somalia 2-0 katika mchezo
wa kwanza wa kundi hilo kwenye Uwanja huo.
Mabao
ya Burundi yalifungwa na Abdoul Fiston dakika ya 40 na Nduwarugira Christopher
dakika ya 55.
Mchezo wa pili wa Kundi B unatarajiwa kufanyika jioni hii kati ya Bara na Zambia kwenye Uwanja huo huo.
Mchezo wa pili wa Kundi B unatarajiwa kufanyika jioni hii kati ya Bara na Zambia kwenye Uwanja huo huo.
Kikosi cha
Stars kilikuwa; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan,
Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk89, Hassan
Dilunga/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk85, Elias Maguri/Haroun Chanongo dk72, Amri
Kiemba na Mrisho Ngassa.