Mganga Geoffrey Wanjala Wechule |
MGANGA
mmoja wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Geoffrey Wanjala Wechule jana ameiambia Mahakama Kuu kwamba “alimuua mwanamke wa miaka
18 kwa sababu alimvuta uume wake walipovua nguo kushiriki ngono.”
Lakini
Jaji Florence Muchemi alimwamuru Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP)
Keriako Tobiko awasilishe ushahidi katika kesi hiyo.
Jaji
Muchemi alimweleza Geoffrey Wanjala Wechule ushahidi utawasilishwa kortini
ndipo “ korti iamue ikiwa yuko na kesi ya kujibu au la.”
Bw
Wechule mwenye umri wa miaka 36 alikiri alimuua Jane Kadogo Mutiso siku
kuu ya Mashujaa Oktoba 20 katika eneo la Gitina mtaani Kawangware Kaunti ya
Nairobi.
Tangu
afikishwe kortini Oktoba 22 mshtakiwa “ amedumisha kusema kwamba alimuua
Kadogo na yuko tayari kufa.”
Hata
jana alikariri “nilimuua Kadogo. Nilikuwa na sababu ya kumuua.”
Aliposomewa
shtaka Jaji Muchemi alimwuliza , “ Unasemaje kuhusu shtaka inayokukabili.
Ulimuua Jane Kadogo Mutiso au hakumuua?”
“
Nilimuua Kadogo.Nilikuwa na sababu ya kumuaa,” Bw Wechule akajibu.
“Ulimuua
kwa sababu gani,” Jaji Muchemi alimtaka aeleze.
“
Nilimuua kwa sababu alivuta uume wangu. Alinivuta sehemu zangu nyeti,”
mshtakiwa alimjibu Jaji Muchemi.
“
Hii korti imechukulia kwamba umekana shtaka. Nimeandika kwamba umekana shtaka
ijapokuwa unakiri. Lazima DPP awasilishe ushahidi ndipo uamuzi utolewe,” Jaji
Muchemi alimweleza mshtakiwa.
Mahakama
iliamuru Kesi hiyo itajwe Desemba 9, 2013 maagizo zaidi yatolewe.
Jaji
Muchemi aliamuru mshtakiwa azuiliwe katika gereza la Viwandani hadi siku hiyo.
Mahakama
iliamuru kiongozi wa mashtaka Daniel Karuri amkabidhi mshtakiwa nakala za kesi
ndipo aandae tetezi zake.
Bw
Wechule anadaiwa alimuua Kadogo alipokataa kushiriki mapenzi naye siku kuu ya
mashujaa licha ya kwamba walikuwa wamekubaliana na hata walikuwa wamevua nguo
wakabaki uchi wa mnyama.