Baadhi ya vipodozi vilivyokamatwa |
Mifuniko ya tenki la mafuta ikiwa imefunguliwa baada ya kutolewa vipodozi |
Ndani ya lori hilo baada ya kutolewa vipodozi hivyo |
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akionyesha shehena ya vipodozi ambavyo vimekamatwa vikisafirishwa ndani ya lori la mafuta leo |
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ,Ramadhan Mungi akionyesha lori la mafuta lililokuwa na shehena ya vipodozi |
Jina la kampuni linalomiliki lori hilo |
Maofisa wa mamlaka ya chakula na dawa Manispaa ya Iringa wakikagua vipodozi hivyo |
JESHI
la polisi mkoa wa Iringa limewakamata watu wawili akiwemo
dereva wa tenki la mafuta lenye namba za usajili T 247 BHP
wakisafirisha shehena ya vipodozi maboksi 779 vikiwa vimewekwa ndani
ya tenki hilo la mafuta kutoka nchi za kusini mwa Tanzania
kuelekea jijini Dar es Salaam .
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa lori
hilo lenye namba za usajili T 247 BHP likiwa na tela lenye namba T
598 BMK ni mali ya kampuni ya World OIL Ltd ya Jijini Dar es Salaam
lilikuwa likiendeshwa na Mohamed Sadru (23) mkazi wa Mbezi Temboni
jijini Dar es Salaam .
Mbali ya dereva huyo pia jeshi hilo linamshikilia
mfanyabiashara aliyekuwa akisafilisha mzigo huo Bw Kassim Kaifa (23)
mkazi wa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika na mzigo huo.
Kamanda
Mungi aliwaeleza wanahabari leo kuwa mtego wa jeshi la polisi
uliweka baada ya kupokea taarifa kutoka kwa rai wema kuhusiana na
lori hilo kutumika isivyo kwa kusafirisha vipodozi hivyo.
Alisema
kuwa taarifa kuhusiana na lori hilo kusafirisha vipodozi badala ya
mafuta waliitapata kutoka jana na mtego wa kulikamata lori
hilo umefanikiwa majira ya saa 9 alfajiri ya leo
Hata
hivyo alisema kuwa sehemu kubwa ya vipodozi hizo ni vile
ambavyo vilipigwa marufuku na serikali kutokana na kuwa na madhara
makubwa kwa afya ya watumiaji wa vipodozi hivyo.
Alisema
kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kumata vipodozi hivyo kwa
kushirikiana na mamlaka ya chakula na dawa ,wakala wa barabara mkoa
wa Iringa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
Kamanda
huyo alisema kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara
baada ya uchunguzi kukamilika na kuwa ni mapema kwa sasa kuitaja
thamani ya vipodozi hivyo na nchi ambayo lori hilo lilikuwa
likitoka kutokana na sababu za kiusalama.
Na Francis Godwin Blog