|
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo eneo la Mtwivila |
|
Mume wa marehemu Bw Hamza Kidava na mtoto wake wakitoa heshima za mwisho kabla ya mazishi |
|
mwili wa marehemu Doris Lyandala |
|
Kaburi la marehemu Doris |
|
Aliyekuwa mume wa marehemu Doris Lyandala Bw Hamza Kidava kushoto akiwa na rafiki zake nyumbani kwao Mtwivila leo |
|
Bw Hamza Kidava akiwa katika majonzi mazito |
|
Bw Hamza Kidava akionyesha eneo ambalo mke wake kipenzi alipouwawa kwa kuchomwa visu na mtu anayesadikika kuwa ni kichaa |
|
Bw
Hamaza kushoto akimwonyesha mwandishi wa mtandao huu mzee wa matukio
daima hayupo pichani na Bw Brown eneo ambalo mke wake aliuwawa |
|
Dereva
Taxi aliyekuwa akimwendesha Mzee wa matukio daima Bw Brown akiwa
nje ya nyumba aliyekuwa akiishi mtuhumiwa wa mauwaji ya Bi Doris
Lyandala HAKUNA Kati yetu ajuaye siku yake na kufa na kifo chake
kitakuwaje na kama ungelijua lijalo mbele yako hakuna ambaye
angejaribu kutoka ndani ya nyumba yake kwenda kukutwa na mauti. Ni
kauli za majirani na marafiki wa karibu wa mrembo
Doris Lyandala ambae kwa sasa kwa wakazi wa mji wa Iringa jina lake
ndilo limeendelea kutesa mawazo ya wengi. Doris ambae enzi za uhai
wake alipata kuwa mmiliki wa Saloon yake ya kutengeneza nywele
warembo wenzake na alipata kuwa mcheshi asiyependa makuu tulitamani
tungekula na kusherekea nae pamoja Krismas ambapo ilibaki siku moja
pekee kula Krismas na rafiki ,familia yake na zilibaki siku takribani
7 kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 ila yote hayakuwezekana
na badala yake rafiki na ndugu walijikuta katika simanzi ya kifo
chake . Mmoja kati ya marafiki zake wa karibu Salima Alli alisema
kuwa alikuwa ni mteja wake mkubwa katika saloon na kabla ya kukutwa
na umauti siku moja kabla alipata kumseti nywele zake. Bw Hamaza
Kidava ndie mume wa marehemu huyo anasema kuwa alipata taarifa
kutoka kwa majirani kuwa kipenzi chake mke wa mtoto mmoja amepatwa na
tatizo na amekimbizwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa. Alisema
kuwa baada ya kufika Hospital hapo hakuamini kuona mke aliyempenda
kuliko akitokwa na damu huku akieleza kwa shida kilichomkuta . Akizungumza
kwa uchungu mwigi huku akilengwa na machozi Hamza ambae ni mmoja kati
ya vijana watanashati na wenye ajira zao akiwa katika sekta ya
kutengeneza simu alisema kuwa alichoelezwa kuwa amechomwa visu na
kichaa. "Ina niuma sana kumpoteza mke wangu na ina niuma sana
kuona leo nimebaki mpweke nikilea mtoto mmoja ambae nimezaa nae mke
wangu Doris ....kaka nashukuru kwa kuja kunifariji na nawashukuru
wote walioshiriki kuuguza hadi mazishi yake "alisema Hamaza kumaliza
kwa kusema twende nikakuonyeshe alipokutwa na mkasa huo wakati akitoka
dukani kutafuta mahitaji. Ndudu wa karibu na mtuhumiwa wa mauaji
hayo ambae hakupenda jina lake kuandikwa hapa kwa kuwa si msemaji wa
familia alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa mauwaji Bw Zakayo Lwambano
(26) ni mkazi wa Mtwivila na alikuwa akiishi mtaa mmoja na marehemu
Doris . Alisema kuwa kijana huyo Zakayo alianza kuugua ugonjwa
huo toka mwaka 2010 ambapo ndugu walimpeleka Hospital ya vichaa Milembe
Dodoma na kurejea akiwa mzima wa afya. Hata hivyo alisema baada
ya kurejea alikuwa ni mtu aliyetulia na kujipatia kipato chake cha
kila siku kwa kufanya kazi ndogo ndogo za kusomba mchanga na nyingine
kwa wananchi wa eneo hilo . Ndugu huyo alisema wazazi wa mtuhumiwa
huyo kwa sasa walisha fariki dunia na alikuwa akiishi peke yake katika
getho ( nyumba yake ya chumba kimoja ) aliyojenga mwenyewe Alisema
kuwa siku ya tukio Desemba 24 kabla ya kumshambulia Mrembo huyo
alianza kumchoma kisu ndugu yake James Moyo (28) ambae alifika
nyumbani hapo kwa ajili ya kula sikukuu akitokea Makambako Njombe. Alisema
kijana huyo aliyejeruhiwa alikuwa akiishi nyumba nyingine tofauti na
getho la mtuhumiwa na alichomwa visu viwili kwapani na kukimbizwa
Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa na kwa sasa ameruhusiwa na kurejea
Makambako kwao. Pia alisema mtuhumiwa huyo baada ya mauwaji alijipeleka mwenyewe polisi na kutaka awekwe ndani kwa madai ameua Jeshi
la polisi mkoa wa Iringa limethibitisha kutokea kwa mauwaji hayo na
kuwa mtuhumiwa huyo hadi sasa anashikiliwa na polisi . Kamanda wa
polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa mwanamke
huyo alichomwa visu sehemu mbali mbali ya mwili wake na baada ya
kukimbizwa Hospital akiendelea na matibabu alifariki dunia. Alisema
kuwa mtuhumiwa huyo amenashikiliwa kama watuhumiwa wengine na kuwa
mwenye mamlaka ya kumfunga ama kutomfunga ni mahakama na wao kama
polisi hawajui kama ni kichaa wanajua kama mtuhumiwa wa mauwaji. Mtandao
huu na wadau wake unatoa pore nyingi kwa familia ya Kidava na
Lyandala pamoja na ndugu na jamaa wote ambao wameondokewa na mpendwa
wao ambae sote tulimpenda sana ila Mungu kampenda zaidi yetu hivyo
hatunabudi kusema jina lake lihimidiwe milele yote |
Chanzo;Fransis godwin blog