Home »
Uncategories »
MAN WALTER AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA NYIMBO ALIZOMTENGENEZEA LADY JAYDEE, SOMA HAPA KUJUA
MAN WALTER AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA NYIMBO ALIZOMTENGENEZEA LADY JAYDEE, SOMA HAPA KUJUA
Unknown
4:06 PM
Producer wa Combination
Sounds, Man Walter amesema kufanya kazi na Lady Jaydee aliyemtayarishia
hits zake mbili, Joto Hasira na Yahaya ni kitu kilichomsogeza mbele
katika career yake.
“Kufanya
kazi na msanii mkongwe na ukazidi kumsogeza pale ambapo alifikiria
kufika inakuwa ni faraja sana kwa maana na mimi nimeongeza kujiamini
kwamba naweza pia kufanya maajabu zaidi, sababu mwanzoni ilikuwa ni
ndoto kufanya kazi na Jaydee, nilikuwa napenda. Nashukuru nimefanya na
nimefanya vizuri,” Man Walter aliyetajwa mwaka huu kuwania tuzo ya Mtayarishaji Bora wa muziki wa kizazi kipya ameiambia Bongo5. “Hata kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Kilimanjaro Music Awards kunanifanya nijifariji na ni ngoma ambazo ninazitegemea sana.”
Walter amesema bado anaendelea kufanya kazi zingine na Lady Jaydee. “Projects
zake nyingi ni kama amezihamishia Kombinenga. Nashukuru sana kwa hilo
kwasababu ametokea kuniamini sana mpaka kunipa kazi nyingi ambazo
nitazifanya,” amesema.
Producer
huyo amesema kazi za wasanii wengine zitakazotoka kwenye studio yake ni
pamoja na ile ya Christian Bella aliyomshirikisha Ommy Dimpoz. Wimbo
huo amesema ni maalum kwa wanawake na unatarajiwa kutoka hivi karibuni
huku akidai kuwa ni lazima utafanya vizuri.
>>BONGO5