WAZIRI PROF. MARK MWANDOSYA ALITAARIFU BUNGE LA KATIBA KUHUSU AJALI YA HELKOPTA ILIYOMPATA MAKAMU WA RAIS NA UJUMBE WAKE

Waziri Prof. Mark Mwandosya ametoa taarifa bungeni mjini Dodoma kuhusu ajali ya helkopta iliyomkumba makamu wa rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal na ujumbe wake jana na kusema wamepata majeraha madogo madogo lakini si ya kutisha. 
Prof. Mwandosya amesema ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa wote waliokuwa kwenye helkopta hiyo wamenusurika kifo na wapo salama salimini. 
Amesema maeneo mengi ya nchi yamekumbwa na maafa ikiwemo Dar es salaam, Pwani, Morogoro na mikoa mingine yamekumbwa na mafurikio ikiwemo kuharibika kwa miundombinu hasa ya barabara na serikali imeshaanza jitihada za kuhakikisha miundombinu hiyo inatengenezwa mara moja na kurudi katika hali yake ya kawaida. 

Pia waziri Mwandosya amependekeza posho ya leo ya wabunge wa bunge maalum la katiba kujitolea posho ya leo ili iwe maalum kwa waathirika wa mafuriko sehem mbalimbali za nchi. 

Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo Mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Mh. Samwel Sitta amesema suala hilo litaenda kujadiliwa kwenye kamati maalum ambayo ina kikao chake leo na itatoa taarifa kwa bunge mara baada ya kujadili


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...