MBUNGE MKOSAMALI NUSURA APIGANE NGUMI NA MKUU WA WILAYA,SHUHUDIA HAPA



MKUU wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Venance Mwamoto, amevamia jukwaa la mkutano wa NCCR-Mageuzi na kisha kumtolea lugha ya matusi Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali.

Mwamoto alijikaribisha kwenye mkutano huo uliokuwa ukihutubiwa na Katibu Mkuu, Mosena Nyambambe kisha akaketi kiti cha mbele walipokuwa viongozi wengine wa chama hicho na kuanza kumchokoza Mkosamali kwa kumtolea 

lugha chafu kwa sauti ya chini.

Mkuu huyo wa wilaya anadaiwa kufikia hatua hiyo ya kuporomosha matusi kwa kilichoelezwa 
kuwa alituhumiwa na Mkosamali kwenye mkutano, kwamba amejimilikisha isivyo halali ekari 73 za ardhi katika Kijiji cha Nduta wakati tayari anatumia wanajeshi kuwaondoa wanakijiji hao kwa kile kilichodaiwa ni kutaka kubadili matumizi ya ardhi ili kijiji hicho kiwe hifadhi.

Sokomoko hilo lilimalizwa kwa busara za wabunge, David Kafulila (Kigoma Kusini) na Moses Machali (Kasulu Mjini) baada ya Mwamoto na Mkosamali kukaribia kuzichapa kavu kavu jukwaani


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...