Kupomomoka kwa jengo la ghorofa tatu
ndani ya Westgate Mall baada ya mlipuko uliosababisha vifo vya magaidi
wa 5 na na wengine 11 kushikiliwa na Polisi siku ya Jumatatu Sept 23,
2013 kama unavyoonekana katika picha magari yaliyokua yameegeshwa juu
ya paa la magesho ya magari yakiwa yameanguka chini kwa mlipuko huo.
Paa la maegesho ya magari likiwa limebomoka kutokana na mlipuko huo.
Wananusalama wakijadili jambo baada ya
jaribio hilo la Westgate Mall kuzimwa baada ya mlipuko uliosababisha
jengo la ghorofa 3 kuporomoka baada ya magaidi wa Al Shabab kuvamia
Mall hiyo siku ya Jumamosi Sept 21, 2013 na kusababisha vifo nya watu
69 na wengine 175 kujeruhiwa huku kikundi hicho cha Kigaidi kudai
kwamba hawataishia hapo mpaka Kenya itakapoondoa majeshi yake Somalia.
Picha za nje ya jengo la Westgate hazioneshi uhalisia wa hali iliyoko ndani ya jengo baada ya shambulio la kigaidi Jumamosi iliyopita jijini Nairobi, Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 70. Picha hizi zinatoa picha halisi ya jinsi jengo hilo lilivyoharibika vibaya kwa ndani baada ya ghorofa tatu za jengo hilo kudondoka baada ya kupigwa mabomu katika mchakato wa kukabiliana na magaidi. Hivi ndivyo jengo la West gate linavyoonekana kwa nje
Picha hizi pia zinaonesha jinsi magari yaliokuwepo eneo la maegesho ya magari katika jengo hilo yakiwa yameharibiwa kiasi kwamba kuna mengine ambayo huenda hata wamiliki wanaweza kushindwa kuyatambua. Picha: Nairobi Wire, Mail Online