RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA LALA SALAMA YA KAMPENI CHALINZE‏

 6
Mgombea Ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mkoko katika mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo.
7
Wananchi wakiwa wamejikinga jua na picha ya mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete.
3
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi bendera Bw Iddi Mjema aliyekuwa mwenyekiti wa CUF kata ya Msata baada ya kurudisha kadi ya CUF na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM jana wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Pongwe Msungula kata ya Msata jana, katikati ni Meneja kampeni na Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Bw. Kazidi. Uchaguzi wa jimbo la Chalinze unatarajiwa kufanyika Aprili 6 Jumapili mwaka huu.
4
Sam wa Ukweli akiimba na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha
Mkoko.
5
Mmoja wa wananchi akiwa amejikinga jua na picha ya mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete.
9
Mwanamuziki Hafsa Kazinja akiimba na wananchi katika mkutano wa kampeni katika kijiji cha Madesa.
10
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete akicheza na akina mama katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Madesa kata ya Msata.
11
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Kihangaiko.
12
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM akicheza pamoja na Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete wakati akimnadi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Lugoba jana.
13
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana mkoa wa Simiyu Bw. Njalu Silanga wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Lugoba.
14
Mbunge wa Shinyanga mjini na Naibu Waziri wa Madini Mh.Steven Masele akimuombea kura Bw. Ridhiwani Kikwete katika mkutano wa kampeni uliofanyika Lugoba jana.
15
Wananchi wakinyoosha mikono yao juu kama ishara ya kumkubali mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete.
2
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete akiangalia bendera ya Chama cha kampeni ya CUF iliyokabidhiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Msata mara baada ya kujiunga na CCM katika kijiji cha Pongwe Msungula kwenye mkutano wa chama cha Mapinduzi.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...