Linex achoshwa na maswali yanayomhusu Jackie Cliff kwa kuwa alifanya nae video, ayatolea majibu kwa ujumla

Mwimbaji wa Kimugina, Linex Linenga amesema amechoshwa na kufuatiliwa na kuulizwa maswali mbalimbali  kuhusu uhusiano wake na Jackie Cliff ambaye alikuwa Video Queen kwenye wimbo wake ‘Kimugina’,  mrembo aliyekamatwa nchini China hivi karibuni na dawa za kulevya aina ya Heroin zenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania milion 220.
Linex ameutumia ukurasa wake wa facebook kutoa ufafanuzi wa jumla kuhusu uhusiano wake na mrembo huyo.

Linex ameandika:
Nimechoka maswali kuhusu jack cliff model nilieshoot nae kimugina napenda kuwambia wote wanaoniuliza maswali ya ajabu kwamba sijawah kua na ushikaji na jack zaid ya kumtafuta nilipokua na kazi nae so sijui kitu chochote kuhusu jack anafanya nn ana nn ana kaz gan zaid ya umodel sijui so mnaonitupia maswali na picha wats up plzzz cos sijawahi kua karibu na Jack na sijui chochote kuhusu jack zaidi ya kufanya nae vdeo.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...