MANJI AKUBALI KIPIGO CHA 3-1 MTANI JEMBE
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, akiongea na wanahabari (hawapo pichani). MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amekubali kipigo cha 3-1 kutoka kwa Simba na kusema asitupiwe lawama mchezaji wala kiongozi yeyote kwa matokeo ya jana. Manji ameyasema hayo leo wakati akiongea na wanahabari katika makao makuu ya timu yake yaliyopo Mtaa wa Twiga na Jangwani baada ya mechi ya jana ya Watani wa Jadi, Simba na Yanga, kwenye mchezo wa ‘Nani Mtani Jembe’ uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-1. Manji ameongeza kuwa kama ni lawama basi alaumiwe yeye maana ndiye kiongozi wa timu.