Wasafiri walilazimika kutembea kwa umbali mrefu kidogo ili kumuachia dereva aendeshe katika hali yeyote ngumu kufuatia mafuriko makubwa yanayotokana na kutokamilika kwa miundombinu ya barabara hiyo inayotokea mjini Tabora kwenda Nzega kupitia Ipuli
Haikujalisha cha mrembo wala cha nani; ni kuvua viatu na kutembea majini.
Abiria wakizionja adha hizo vizuri kwa kukanyaga kipande kirefu kwa miguu kupisha sehemu mbaya iliyoharibika vibaya baada ya mvua kunyesha. Barabara hii bado inaendelea kutengenezwa kwa kiwango cha lami
Abiria wakilikwamua gari baada ya kunasa. Haikwepeki kazi hii ikiwa inakulazimu usafiri bila kujali ubovu wa barabara
Dimbwi kubwa la maji ya mvua
Gari la kampuni fulani likiwa limekwama
Hii ni ajali ya gari la mizigo ambalo inadaiwa ilitokea huku abiria wakilishuhudia mbele yao kwa macho yao moja kwa moja likipinduka gari hilo.
Hakika wawezajiuliza ikiwa isingelikuwa ubovu wa barabara lingepinduka gari hili...?
Ni adha kubwa sana kwa karne hii watu kuendelea kulia na tatizo la barabara mbovu, ikiwa ni moja ya mikoa maarufu nchini Tanzania ambao hakuna barabara ya kiwango cha lami inayounganisha mkoa huo na mikoa mingine.
Mkoa wa Tabora una barabara nyingi zinazounganisha mikoa mingi ya Tanzania ukitokea Tabora-Mwanza, Tabora-Singida, Tabora-Mbeya, Tabora-Arusha, Tabora-Rukwa, Tabora-Shinyanga na kwingineko.