Zitto Kabwe
Nitapambana kutetea uanachama wangu.
Kwa upinzani ni lazima tufanye tofauti na CCM. Tuhuma za matumizi
mabaya ya fedha za umma kwa upinzani ni mbaya zaidi kuliko. Hivyo
uwajibikaji kwa wote bila kujali vyama. Uwajibikaji sio msamiati kwa
watawala tu bali kwa viongozi wote. Namna tunavyotaka nchi iendeshwe ndivyo hivyo tuendeshe vyama vyetu. Tuhuma dhidi ya Kiongozi wa
Upinzani kuhusu masuala ya uadilifu zinapaswa kuhukumiwa kwa namna
ile ile wanayohukumiwa watawala.
Ninarudia kuwaambia ndugu zangu kwamba sitoki CHADEMA. Chama kina
jasho langu na nitapambana mpaka dakika ya mwisho kutetea haki ya
uanachama wangu. Mimi ni CHADEMA toka ujana. Niliingia CHADEMA kwa kuchagua na sio
wengine walioingia kwa Mazingira Ya kupata fursa za kugombea. Wengine
wangepitishwa na chama walichokuwa kuwa wagombea Leo wasingekuwa
upinzani na inawezekana wangekuwa mawaziri mizigo au waendesha
operesheni tokomeza!