WAFANYA BIASHARA MWANZA NAO WAGOMEA MASHINE ZA TRA

Hali hii imeathiri hata wauza magazeti kwani hakuna pilikapilika za wachuuzi na wanunuzi ambazo husababisha wao kupata wateja kwani ni bidhaa inayohitaji wapita njia....
 Wafanya biashara wa maduka ya jijini Mwanza leo wagoma kufungua maduka yao wakigomea mashine za risiti za EFD toka TRA na hii ndiyo hali ya baadhi ya maduka barabara yenye pilika pilika ya Nyerere jijini hapa.
 Hata wale wakala wa magodoro na huduma nyingine zote wamejumuika kwenye mgomo huo.
 Hakuna huduma kabisa mitaa hii ambayo hukusanyisha wanunuzi wa mahitaji ya bidhaa mbalimbali..
 Na maduka ya huduma kwa bidhaa za kielektoniki pamoja na vifaa vya kuendesha mashine na injini imesitishwa kupitia mgomo. 
 Wafanya biashara wa vyombo vya elektoniki nao waunga mkono mgomo huo.
Umekuwa kama mji wa kale uliokimbiwa.
Kweupeeeeee.
HALI ILIVYO KATIKA ENEO LA TANGANYIKA.
Wafanyabiashara wamekutana hapa katika kituo cha zamani cha mabasi cha Tanganyika wakiwa na mabango yao yanayowasilisha ujumbe wa kukinzana na ujio wa mashine hizo ambapo mbali na makato yake pia kodi nyingine hutozwa pembeni hali wanayoitafsiri kama unyonyaji. 

Jijini Mwanza hususani eneo la katikati ya jiji barabara ya Nyerere, Kenyata, Lumumba, Libert na maeneo yote ya wilaya ya Nyamagana leo wafanyabishara wake katika maeneo hayo waliingia katika mgomo wa kutofungua maduka yao kupingamashine za kutolea risiti za elektroniki (EfDs) ambazo zipo katika mfumo wa uhakiki wa ukusanyaji kodi. 

Wafanyabishara hao wamelalamika kuwa mbali na kuwepo kwa mashine hizo za EfDs zinazo hakiki mauzo yao na utozaji kodi lakini pia wamekuwa wakiongezewa kodi kila kukicha.

Wamesema kuwa matatizo ya mashine hizo ya kuharibika mara kwa mara, kushindwa kutoa mahesabu ya siku kwa wakati na kushindwa kuprint risiti ni kero kwao.


Kufuli. PICHA ZOTE na Sammy Poneka.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...