Kama
unaingia kwenye kikao, unatakiwa uonyeshe uwezo wako wa kuchangia ili
mambo yaende vizuri na kuwa bora zaidi, usiongee vitu vya kukatisha
tamaa au visivyokua na tija.
1. Ngoja nikupe rejea kuhusu jambo hilo...
Rejea
sio jambo baya kama ni nzuri na imefanywa vizuri inasaida kundi kupata
suluhisho la jambo fulani, lakini wakati mwingi mtu akisema anataka
kutoa rejea ya kitu fulani ni kujaribu kutupilia mbali maswali, kama
hauko tayari kutoa suluhisho ya jambo fulani ruhusu mazungumzo yaendelee
mbele na rejea hiyo kaa nayo mwenyewe.
2. Nimeshatuma Barua Pepe
Mazungumzo
ya Uso kwa Uso hayatakuwa na maana kama ukisema umeshatuma barua pepe
na kila mmoja akasome. Badala yake ongelea kwa muhtasari suala hilo ili
kila mmoja ajue ni kitu gani kinaendelea.
3. Hilo si jambo la msingi sana.
Maneno
kama hayo hutokea mara nyingi, ukisema jambo si la msingi, kwanini?
Hata kama jambo linaloletwa mezani si la wakati huo haimaanishi
lisichuKUliwe umaanani. Kwa mwingine kwenye kitengo chake ni jambo la
muhimu sana.
4. Hakuna anayekubaliana na Hilo
Kwenye
kikao inatakiwa kila mtu atoe mchango wake na mawazo yake. Kama kuna
mtu anakuja na kauli hiyo unatakiwa kuwa makini, inawezekana ni kweli au
aliyekuja na kauli hiyo kuna kiTu kinaendelea ambacho wewe hukijui.
Mara nyingi wazo zuri ni lile kila mtu anafikiri litashindwa vibaya.
Ukiona vipi, angalia kwa ukaribu zaidi kile watu wengi wanaonyesha
hawakipendi.
5. Hakuna wazo baya.
Wakati
hutakiwi kukatilia mbali wazo ambalo kila mmoja halipendi, hakuna wazo
baya, wazo baya huja kutoka kwa watu ambao hawakuwepo kwenye kikao. Kama
utaruhusu wafanyakazi wakawa huru kutoa mawazo yao, utapunguza
majadiriano yasiyokuwa ya msingi.
6. Mimi ndo kiongozi hapa
Hiyo
ni kauli ya kuondoa mawazo, kutawala watu waliohudhuria kikao au
unataka kurudisha mambo kwenye mstari. Hiyo inaweza kuwa taa nyekundu
kwamba mtu huyo anajiona hana madaraka au kikao hicho si cha majadiliano
hasa.
7. Ngoja tutafute Mtaalamu mzuri
Vikao
ni kwaajili ya majadiliano, unapoongea kwamba hapo hakuna mtu mwenye
ujuzi ambaye anaweza kuongea suala fulani unasababisha na kunyamazisha
mjadala mahala hapo. Inawezekana una mawazo kuhusu mtu nje ya hicho
kikao ila unapotoa kauli hiyo unajiweka matatani. Unakuwa ni mtu mwenye
kutilia mashaka kila mtu unayefanya naye kazi.
8.Tutakuwa na Kikao cha ufuatiliaji
8.Tutakuwa na Kikao cha ufuatiliaji
Hiyo
ni mbaya zaidi, kwani kikao ulichopo sasa kazi yake ni nini? Ni vizuri
ukisema kikao cha ufuatiliaji hakitakuwepo kwa kuwa mtu husika wa jambo
hila atakuwa akitupasha haLi kwa kila kinachoendelea.
Je una mawazo yako binafsi ? Haukubaliani? Usisite kutuandikia mawazo na mchango wako