Mrembo
anayedaiwa kuwa Jack Patrick (akiwa amefunikwa uso) mikononi mwa polisi
nchini China baada ya kukutwa na pipi 66 za heroin tumboni.
Mwanamitindo Jack Patrick.
Mrembo
anayedaiwa kuwa Jack Patrick akipelekwa katika chumba maalum kwa ajili
ya mkutano na wanahabari Jumanne Desemba 19, 2013 huko Macao China. Polisi wakichunguza pipi zenye dawa za kulevya alizokutwa nazo mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick. Wanahabari nchini China wakichukua picha za dawa hizo za kulevya anazodaiwa kukutwa nazo Jack.
MODO maarufu Bongo, Jacqueline Patrick Cliff, anadaiwa kukamatwa na
kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao nchini China. Dawa
hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray
ambapo alikutwa na jumla ya pipi 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani
137,720 sawa na shilingi milioni 215.5 za Kitanzania.Inadaiwa kuwa Jack alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne ya Desemba 19, 2013. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko China.
Jack alipata jina aliposhika namba tatu kwenye Miss Ilala na kushiriki Miss Tanzania mwaka 2005/06. Pia uliuza nyago kwenye video ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marehemu Albert Magwea ‘Ngwair’ iliyokwenda kwa jina la She Got A Gwain. Kuanzia hapo jina likawa kubwa na akawa mwanamitindo maarufu Bongo.
Ni katika kipindi hicho cha umaarufu akaolewa na mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Abdallah Fundikira, Abdulatif kabla ya jamaa huyo kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Keko, Dar akikabiliwa na msala wa kusafirisha mihadarati.
GPL