MANCHESTER UNITED YAONDOLEWA CAPITAL ONE CUP KWA MATUTA

Shangwe: Wachezaji wa Sunderland wakishangilia kutinga fainali baada ya kuwaondoa Man Utd.
Majonzi: Wachezaji wa Manchester United wakiwa na nyuso za huzuni.
Kifo cha nyani: Rafael wa Man Utd akikosa penalti iliyowapa ushindi Sunderland.
Tukutane Machi 2 Wembley: Sunderland wakiwashukuru mashabiki wao 9,000 waliofika uwanjani kuwashangilia na kuwaomba wakutane Wembley katika fainali na Manchester City.
TIMU ya Manchester United imeendelea kusuasua katika michuano mbalimbali baada ya kuondolewa na Sunderland katika nusu fainali za michuano ya Kombe la Ligi maarufu kama Capital One Cup iliyopigwa Old Trafford.
Manchester imetupwa nje ya mashindano hayo kwa mikwaju ya penalti baada ya matokeo ya awali kuwa sare ya 3-3 na Sunderland kushinda kwa penalti 2-1.
Baada ya matokeo hayo, Sunderland inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi 18 juu ya Cardiff City katika Ligi Kuu ya England, itakutana na Manchester City Machi 2 mwaka huu katika fainali itakayopigwa uwanja wa Wembley.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...