CHUKUA tano! Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amefanikiwa kumpatanisha Jacqueline Wolper Massawe na mbaya wake ambaye ni msanii mwenzake wa filamu (jina kapuni).
Akizungumza na gazeti hili, Steve alifunguka kuwa uongozi wake upo kwa ajili ya kuweka kundi hilo likae katika njia sahihi hivyo aliamua kumuita Wolper na huyo msanii mwenzake ambapo alifanya nao kikao cha saa kadhaa maeneo ya Mbezi Beach, Dar.
Alisema kuwa alifurahishwa kuona bifu hilo limekwisha kwani yeye anapenda watu wapendane na kundi liwe na amani, kusiwe na mifarakano ya hapa na pale ndiyo maana alichukua jukumu hilo na sasa wako vizuri.
Kwa sasa wawili hao wanazungumza tofauti na zamani ambapo walikuwa hawasalimiani hata wakikutana uso kwa uso.
“Nimefurahi sana kwa kuwa nimeweza kuwapatanisha, haikuwa kazi rahisi lakini nimefanikiwa, naamini wataendelea kuzungumza vizuri na kupendana maana mimi ni mtu wa amani, napenda na wasanii wangu wawe na amani na wapendane pia,” alisema Steve ambaye naye amepatana na Wema Sepetu baada ya kuwa Mwenyikiti wa Bongo Movie Unity.
Wolper na msanii huyo waliingia kwenye gogoro zito baada ya mbaya wake huyo kumkashifu Wolper laivu runingani na kumshambulia kwa maneno makali
GPL