WANANCHI WAZUIA MSAFARA WA RAIS KIKWETE KWA MABANGO

Msafara wa JK ukiwa umezuiwa eneo la Mbwila Ludewa leo



 Wananchi  wa Mlangali  wakiwa  wamezuia  msafara wa Rais Kikwete
 Madai  ya  wana Ludewa kwa JK

Msafara  wa JK  ukiwa  umezuiwa  eneo la Mbwila Ludewa leo

 Mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kushoto  akisaidia  kueleza  kero za wana Ludewa kwa Rais Kikwete baada ya msafara  wake  kuzuiwa  eneo la Mlangali  leo
mwandishi  wa habari wa TBC Mbeya  Bw Hosea Cheyo akiondoka  eneo la  tukio katika  Hospital ya Ludewa   baada ya  maofisa  usalama wa Kikwete  kutimua  wanahabari wasio kuwa na vitambulisho  vya Ikulu jambo ambalo limepingwa na  wahabari kuwa ni unyanyasaji mkubwa  
MBUNGE  wa  jimbo la Ludewa  Deo  Filikunjombe  awafyatua  mawaziri mbele ya  Rais Jakaya  Kikwete  kuwa  wamekuwa  wakitembelea  jimbo lake la Ludewa wakati wa ziara ya Rais na waziri mkuu   wakati  siku  zote  wananchi  wa  jimbo  hilo  wanalia kwa kero mbali mbali.
 
Mbali ya  kuwawasha mawaziri hao  pia  mbunge Filikunjombe amesema  kuwa  kero ya maji katika mji  wa Ludewa ni kubwa na wananchi kwa zaidi ya wiki moja  sasa hawana maji yamefungwa kwa ajili ya kuelekea Ikulu kwa matumizi ya  Rais hali  wananchi wa mji huo akiwemo yeye mwenyewe wamekosa maji ya kuoga kwa  zaidi ya siku tatu sasa.
Mbunge Filikunjombe alitoa kauli hiyo leo katika  uwanja wa Ludewa wakati wa mkutano wa hadhara  wa Rais  Kikwete.
Kwani  alisema kuwa  mbali ya jitihada mbali mbali ambazo serikali ya Kikwete  imekuwa ikifanya katika kusukumba mbele maendeleo ya  wana Ludewa kwa kuanza ujenzi wa lami , mradi mkubwa wa makaa ya mawe na mchuchuma  ila  bado  wananchi hao  hawana shaka na miradi  hiyo isiyo kuwa wanataka  miradi  hiyo inanze  kuwanufaisha  wana Ludewa hata kwa ajira badara ya  wageni kutoka Kenya kupewa vitalu katika migodi  hiyo  huku  wakazi  wa Ludewa  wakipokonywa vitalu  vyao.
Hata  hivyo alisema  kuwa  ni vema miradi  hiyo kuanza kwa kuwanufaisha wana Ludewa kwanza hata kwa ajira  badala ya kuwatazama  wageni  kutoka Kenya ambao  wamekuwa  wakipewa  vitalu katika miradi  hiyo .
“Mheshimiwa Rais sisi  Ludewa si kama Mtwara  ambao  walisema gesi haitatoka  Mtwara ….sisi Liganga na mawe yatatoka kwenda  mikoa mingine  ila tunataka   vijana wa Ludewa waanze  kunufaika kwa ajira “
Pia  mbunge  huyo alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya mawaziri akiwemo  waziri wa nishati ambae amekuwa akifikia  wilaya ya Ludewa  wakati  wa ziara ya Rais badala ya kujenga utamaduni wa kuwatembelea  wananchi mara kwa mara.
Alisema  wananchi wa Ludewa wamekuwa na kero kubwa  juu ya madini yao kwa  wenyeji  kupokonywa vitalu vyao na ofisi ya madini kanda nay eye kama mbunge amepata  kufika ofisi ya waziri  husika ila hakuna jibu la maana  analolitoa kwake .
Hivyo kumwomba  Rais Kikwete  kuwabana  mawaziri hao  ikiwezekana ofisi ya madini kujengwa  Ludewa na sio Mbeya kama ilivyo sasa.
Awali naibu  waziri wa maji Dr Binilith Mahenge  alimweleza  Rais Kikwete  kuwa wizara  imetenga bajeti  kwa ajili ya kufikisha maji katika vijiji mbali mbali vya wilaya ya Ludewa pamoja na eneo la mji wa Ludewa
Huku  kwa upande wake  naibu  waziri wa nishati na madini  George Simbachawene alisema  kuwa  wizara  yake  itaendelea  kuwahudumia wananchi  wa Ludewa na kuwaomba  viongozi wa wilaya  hiyo kuandaa ukumbi ili  wataalam  wake kuja kukutana na wananchi kwa ajili ya kupokea  kero  mbali mbali.
Wakati  huo  huo wananchi  wa kata  ya   Madope  na Mlangali  katika  wilaya ya  Ludewa  mkoani Njombe  wamezuia  msafara  wa  Rais  Jakaya  Kikwete kuomba  kuharakisha  ujenzi   wa barabara  ya  lami  kutoka  Ludewa –Njombe  pamoja na kero ya soko la  mahindi ambayo  wamedai  yameendelea  kuharibika katika  nyumba  zao

Wananchi  hao wakiwa  na mabango  yanayoelezea  kero hizo na nyingine walizuia msafara  huo kwa nyakati tofauti   wakati Rais Kikwete akitokea  wilaya ya Njombe kuelekea makao makuu  ya wilaya ya  Ludewa kwa ajili ya  ziara  yake  ya  siku mbili  wilayani Ludewa.

Kwa  upande  wao  wananchi  wa Madope  ambako ni mpakani mwa  wilaya ya  Njombe na Ludewa  walimwomba Rais Kikwete  kusaidia kijiji  hicho  kupatiwa  kituo  cha afya pamoja
na kuomba umeme , mnara  wa simu  na barabara  ya lami  kutoka Njombe – Ludewa.
Wakati  wananchi  wananchi  wa kata ya  Mlangali wakimwomba  Rais   Kikwete  kuwasaidia  masoko  ya  mazao  yao pamoja na kupatiwa  huduma  ya maji.


Akijibu  kero za wananchi hao Rais Kikwete alisema  kuwa serikali yake  itaendelea  kuwahudumia ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi zake.
Alisema kuhusu suala la mazao kukosa  soko alisema kwa sasa  serikali imenunua mazao  kiasi cha kutosha na kuwa tayari imewataka  watu binafsi kujitokeza kununua mazao hao.
Pia  alisema  suala la barabara  tayari  barabara ya Ludewa – Njombe ipo katika mkakati wa kujengwa kwa kiwango cha lami na tayari ujenzi  huo umeanza katika mji wa Ludewa.
  

Kuhusu suala la maji alisema kuwa kwa kawaida  upo usemi usemao kuwa wageni njoo wenyeji tupone ila ameshangazwa kuona  Ludewa ni tofauti  wageni  wanapokuja ndipo  wananchi wanapata kero ya maji.

" Ila mimi sikupenda  ninapokuja ninyi mkose  maji ....mimi nitaondoka kesho  tu ila  upo mkakati wa serikali wa kutatua kero ya maji mijini na ninawaahidi katika kipindi kifupi kero hii ya maji itamalizika tayari  bajeti ipo na shabaha yetu kutatua kero  hiyo"

Akielezea kuhusu suala la umeme alisema  vijiji zaidi ya 74  vitanufaika na umeme  vijijini vikiwemo vijiji vya Mlangali , Madope na vijiji  vingine  vyote vya njiani  kuelekea  Songea  na tayari mkandarasi amepatikana na kuwataka wananchi kuanza mandalizi ya kuingiza umeme.

Hata  hivyo Rais Kikwete akielezea  kuhusu  ujenzi wa barabara ya lami alisema kuwa kazi hiyo ina kazi zaidi ya moja ikiwemo ya uchoraji ramani na upembuzi yakinifu zoezi ambalo linaendelea  kabla ya  zoezi la tatu  kuanza.


Alisema  kuwa  kwa upande wa Ludewa tayari  Km mbili na nusu zimekwisha jengwa na sasa wasubiri  kuanza ujenzi wa barabara  yote ya Ludewa - NJombe .


Kuhusu ahadi ya  meli ambayo mbunge Filikunjombe alimtaka  Rais  kutolea ufafanuzi alisema kuwa serikali ipo katika mchakato wa kutekeleza ahadi  hiyo.


Alisema kuwa serikali itanunua meli  tatu kwa ajili ya maziwa matatu Tanganyika , Nyasa na Victoria  na kuwa  tayari kupata  meli  zinafanyika na nchi zaidi ya mbili zinataka  kuleta meli   hivyo kuwa na meli mbili kila  ziwa  


Rais Kikwete alimtaka  mbunge  Filikunjombe kuendelea  kufuatilia suala  hilo kwa waziri DR Mwakyembe  ili  kuona  ahadi hiyo inatekelezeka.
 
Credit: matukio daima


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...