Pamoja
na kupelekwa timu B kwa maelezo wakaboreshe viwango vyao, lakini habari
zaidi zinasema wachezaji hao walitumiwa kuihujmu timu hiyo katika
mchezo wa jana.
Baada
ya mchezo wa jana, kocha wa Simba SC Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King
Kibaden’ alisema kwamba kambi yao ya kujiandaa na mchezo huo ilivamiwa
na vijana wakarubuniwa, ndiyo maana timu yake ilicheza ovyo kipindi cha
kwanza na kulala 3-0 kabla ya kuzinduka kipindi cha pili na kupata sare
ya 3-3.
Kibaden
alisema kwamba anashukuru kupata sare na anawaheshimu, Yanga kwa
kucheza vizuri kipindi cha kwanza na vijana wake kwa kucheza vizuri
kipindi cha pili.
Hata
hivyo, Kibadeni alisema mechi ya jana ilikuwa ashinde yeye zaidi ya
mabao matatu, lakini kwa kuwa kipindi cha kwanza wachezaji wake
waliwaachia Yanga mabao matatu, wakamvurugia mipango.
Abdulhalim Humud kushoto ameambiwa akaboreshe kiwango Simba B |
“Wamewaachia,
mimi nasema timu imewaachia wale wamefunga goli tatu. Si timu ya
kutufunga goli tatu sisi Yanga namna ile. Lakini waliwaachia. Nikarudi
mapumziko nikawaambia sawa, mlitaka kuwaachia tatu, basi zinatosha, mimi
niliwaambia hivyo, msiwape nyingi, hizo zinwatosha. Na kweli
zimewatosha, tumerudisha goli tatu,”alisema Kibaden na kuongeza; “Wala
sijafanya kazi nyingine, nimewaambia tatu mlizowapa wachezaji
zinawatosha kwa kutufunga sisi, lakini nyinyi sasa kachezeni mpira,”.
“Nachozungumza,
tumepata sare mimi nashukuru. Wenzetu walitangulia kipindi cha kwanza,
sisi tukazinduka kipindi cha pili, lakini najua, mimi nimezaliwa
Tanzania, mpira wa Tanzania naujua, mpira unachezwa ndani, mpira
unachezwa nje,”.
“Kuna
kazi kubwa sana kuangalia watu wanaovamia kwenye kambi zetu, kwenye
timu zetu, kutaka kuharibu kuwadanganya watoto, hawa watoto bado wadogo
mimi nasema, sasa hivi wanacheza mpira wa kushinikizwa na watu, ndiyo
maana unakuta matatizo tunayoyapata haya,”.
“Sasa
wengine hawajui, lakini mimi nazungumza kwamba matatizo yapo, timu
mliiona kipindi cha kwanza ilifanya vibaya, lakini si kwa kupenda,
nimetoka mapumziko nimeongea maneno machache tu nimebadilisha timu, wale
wamekuja kucheza mpira sasa, kwa hiyo nataka muwaelimishe watu,
wachezaji kucheza mpira ni kazi yao, wawafurahishe wanachama wao,
wawafurahishe wapenzi wao,”.
“Sasa
wakitumiwa na watu wengine kuja kuvuruga hilo ni tatizo. Sasa kuna vitu
mtavisikia baada ya wiki moja au wiki mbili, mimi kila mwenye matatizo
natoa, najua mwisho nitapata timu safi, lakini nashukuru matokeo,
nawaheshimu Yanga wamecheza mpira mzuri kipindi cha kwanza na mimi
nimecheza mpira mzuri kipindi cha pili,”alisema.
Simba
SC iliingia kwenye mchezo wa jana ikitokea Bamba Beach Kigamboni, Dar
es Salaam ambako imekuwa kambi yake tangu wakati wa maandalizi ya msimu,
wakati wapinzani wao, Yanga SC walihamia Pemba kwa ki moja kujiandaa na
mchezo huo kutoka makao makuu yao, Jangwani.
Hadi
mapumziko, tayari Yanga walikuwa mbele kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na
Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza mawili, lakini kipindi cha Simba SC
ikasawazisha kupitia kwa Betram Mombeki, Joseph Owino na Gilbert Kaze.
Matokeo
hayo yanaifanya Simba SC ibakie nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi
Kuu kwa kutimiza pointi 19, huku Azam FC ikiendelea kuongoza ligi hiyo
kwa pamoja na Mbeya City kwa pointi zao 20 kila timu.
Simba
SC imeondoka leo Dar es Salaam kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo
mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani,
Jumatano.