Mashuhuda wa tukio hilo wanasema baada ya watu hao kutekeleza tukio hilo walikimbia kwa miguu kuelekea pasipo julikana.
Afisa wa polisi wa eneo hilo amesema hadi sasa wamefariki watu wawili na wengine kumi wamepata majeraha ya risasi nakukimbizwa hospitali.
Kikundi cha Al Shabaab kiliwahi kuhusishwa na tukio kama hili huko Nairobi lakini hivi sasa limetokea Mombasa.
Maafisa wa polisi wamesema wanaendelea kufanya uchunguzi wa kuwakamata watu hao japokuwa hadi sasa bado hawajapata tetesi yoyote juu ya watuhumiwa hao.
-Regina Iwole