MTANDAO WA KUMTOA JACK PATRICK WAUNDWA, JUX ATAJWA

Na Erick Evarist
FAMILIA ya modo wa Bongo, Jacqueline Patrick aliyenaswa kwa msala wa madawa ya kulevya Macau- China inadaiwa kuunda mtandao kwa ajili ya kufanikisha zoezi la kumchomoa mrembo huyo mikononi mwa vyombo vya sheria.
Jacqueline Patrick.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na familia hiyo (jina lipo), familia hiyo imeanza mchakato huo hivi karibuni hasa baada ya kudadisi kuhusiana na sheria za eneo alilokamatiwa (Macau) kutokuwa kali kisheria tofauti na maeneo mengine ya nchi hiyo kama Hong Kong.
“Wameandaa mikakati thabiti kwani wamegundua Macau ni tofauti na maeneo mengine ya China ambayo ukikamatwa na madawa ya kulevya na kuthibitika kuwa na hatia, hakuna msalie mtume, ni kitanzi tu. Macau sheria zao si kali sana, wanaweza wakafanikiwa kumchomoa hata kwa njia za panya,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
 
Jux.
“Kinara wa mtandao huo ni Jux yule wanayesema ni mpenzi wake Jack ambaye kwa sasa yupo China. Ndiye ambaye juzijuzi hapa aliposti picha mpya za Jack na kusababisha watu wajue mrembo huyo kaachiwa huru.”
Paparazi wetu alimtafuta dada yake Jack ambaye hakupenda kutaja jina lake  ambapo alisema inawauma kutojua hatima ya ndugu yao hivyo wameona bora wajipange kwenda kufuatilia sakata hilo kupitia kwa Jux waliyemtaja kama ni rafiki wa Jack.
“Tunasikia maneno mengi tofautitofauti, inatuuma sisi kama ndugu hivyo tutajichanga na tutawatuma ndugu wawili ili waweze kwenda kushughulikia suala la ndugu yetu. Katika mkakati huu tumepata na baadhi ya marafiki wa Jack ambao kwa sasa sitawataja,” alisema dada huyo.
Hata hivyo, imeelezwa ndugu hao wametahadharishwa kuwa makini kwani licha ya kusikia sheria za Macau si kali sana wasidharau kwani huenda wakawekewa mtego na kujikuta wameingia katika matatizo kama watajaribu kutumia mlango wa ‘uani’ kumtoa Jack.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...