KISA PENZI LA BURE:. MUME WA MTU AKUNJWA LIVE

Stori:Denis Mtima na Gabriel Ng’osha
Shabaash! Jamaa ambaye jina halikupatikana aliyedai kuwa ni mume wa mtu, ameonja joto ya jiwe baada ya kujikuta akikunjwa na mwanamke kisa penzi la bure alilopewa akashindwa kulilipia.
Jamaa anayedaiwa kuwa mume wa mtu akiwa amekunjana na mwanamke baada ya kupewa penzi na kukataa kulipa.
Wakiwa kwenye ‘patroo’ zao za kufichua uovu, makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, walinyetishiwa kuwa kuna tukio la mwanamke na mwanaume waliokuwa wakizichapa.
Kama mshale, OFM ambao huwa hawalazi damu, walifika mara moja na kunasa tukio hilo lililokuwa ndani ya mgahawa ambao mchana huuza chakula na usiku ni danguro.

Timbwili likiendelea na mwanamke akizidi kudai malipo yake.
Katika tukio hilo ilionekana kuwa mwanaume alizidiwa kwani muda mwingi alikuwa amekunjwa kwa nguo yake shingoni na mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Frida.
“Huwezi kwenda hotelini ukala chakula bure. Lazima ulipe. Jamani huyu baba tumekubaliana nimpe huduma kwa shilingi elfu tano, sasa amemaliza shida zake hataki kunipa changu. Hii ni kazi kama kazi nyingine tuheshimiane,” alisema Frida kwa jazba.
...Mpaka kieleweke.
Kwa upande wake, mwanaume alikuwa akiomba asipigwe picha kwani ni baba wa watoto wawili hivyo akitolewa gazetini ataonekana alichepuka.
“Naomba msinipige picha, nikitoka gazetini itakuwa aibu. Nina mke na watoto nitadhalilika,” alisema jamaa huyo.

Hata hivyo, alipofanikiwa kumtoka Frida, jamaa huyo alizingirwa na vijana waliokuwa wakipita eneo hilo huku mwanamke huyo akiendelea kudai chake akijigaragaza na kumwaga radhi.
Baadaye kila mmoja alichukua hamsini zake baada ya mwanaume huyo kuingia mitini kibabe bila kumlipa Frida.

 
...Soo baada ya kutulia.
NENO LA MHARIRI
Utafiti unaonesha kwamba watu wengi walio katika ndoa ndiyo wanaongoza kwa kusaliti hivyo wanandoa tafakarini halafu mchukue hatua


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...