SKANDALI! Prizenta
maarufu Bongo, Maimatha Jesse amejikuta katika wakati mgumu baada ya
kukwaa skendo ya utapeli kutokana na dawa za kukuza maungo anazoziuza
kuwa hazifanyi kazi.
Prizenta maarufu Bongo, Maimatha Jesse akipozi katika duka lake la vipodozi. |
“Maimatha
anatapeli watu na dawa zake, yaani tumepaka mabinti wengi hazitusaidii
chochote, ni wizi mtupu, laki mbili bila chochote kweli roho inauma.”
Baada ya kunyaka madai hayo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Maimatha akakanusha:
“Hao
wamejisikia tu kuongea hata siwafahamu na wala sijawahi kupata kesi kama
hizo, mbona nilishawauzia wengi? Mimi mwenyewe zimenisaidia, wazushi
tu,” alisema Maimatha.