WATU
48 wameripotiwa kuuawa, hoteli mbili, kituo cha polisi na kituo cha
mafuta kuchomwa moto baada ya shambulio lililotokea eneo la Mpeketoni,
Lamu nchini Kenya jana usiku.Kituo
cha Polisi cha Mpeketoni, hoteli ya Breeze View na Taweel ndivyo
vilivyochomwa moto na moshi ulikuwa bado unafuka leo asubuhi .Imeelezwa kuwa washambuliaji walitokomea na silaha na magari ya polisi kutoka kutuo hicho cha polisi baada ya kushambulia.
Awali washambuliaji hao waliteka daladala mbili 'matatu' eneo la Witu kabla ya kufanya shambulio hilo.
Wananchi walikimbilia katika nyumba
zao wakati polisi wakijibizana risasi na magaidi hao ambapo mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo anadai kusikia washambuliaji hao wakisema "ambieni baba yenu atoe jeshi Somalia”wakimaanisha wamwambie Rais Kenyatta aondoe jeshi nchini Somalia.
Makundi ya Al Shabaab na MRC militia yanadaiwa kuhusika na shambulio hilo