Mtu aliyezoeleka: Dunga ameteuliwa kwa mara ya pili kuwa mirthi wa Luiz Felipe Scolari.
BRAZIL
imemtangaza Dunga kwa mara ya pili kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya
nchi hiyo baada ya Luis Felipe Scolari kuachishwa kazi kutokana na
kipigo cha mabao 7-1 kwenye mechi ya nusu fainali ya kombe la dunia
dhidi ya Ujerumani na 3-0 katika mechi ya mshindi wa tatu na Uholanzi.
Kwa
mara ya mwisho Dunda aliyewahi kuwa nahodha wa Brazil mwaka 1994,
aliifundisha Brazil katika fainali za mwaka 2010 nchini Afrika kusini na
alifukuzwa baada ya kushindwa kufuzu zaidi ya robo fainali.
"Kiukweli nina furaha kubwa kurudi tena," aliwaambia waandishi wa habari.
Miaka ya nyuma: Dunga aliingoza Brazil mpaka hatua ya robo fainali ya kombe la dunia nchini Afrika kusini.