Bus
linalofanya safari za kusafirisha abiria kutoka Dar kuelekea Mtwara
lenye Namba za Usajili T 667 CLY Mali ya Kampuni ya 5 Alliance
limenusurika kuteketea na Moto hivi Punde katika Eneo la Mizani iliyopo
Kijiji cha Mnazi Mmoja kata ya Mingoyo Mkoani Lindi.
Shuhuda
wa Tukio hilo anaeleza kuwa Gari hilo lilifika Kituoni hapo likiwa na
abiria na likiwa katika harakati za kupimwa uzito ndio Watu wa Nje
walishuhudia Moto Ukiwaka kutokea Chini ya Gari hilo na Kuwapigia kelele
wenye Bus na kufanikiwa Kuudhibiti moto huo kabla ya Madhara makubwa
kutokea.
Halihiyo
iliwafanya abiria wa Busi hilo kushikwa na Taharuki na kutoka ndani ya
Bus hilo kwa Haraka sana kwa kuhofia kupoteza maisha yao na
maliwalizonazo, Taarifa inaelezwa kuwa hakuna Majeruhi waliotokana na
ajali hiyo na Hata hivyo tatizo lililekebishwa na Bus hilo liliweza
Kuruhusiwa kuendelea na Safari hiyo ya kuelekea Manispaa ya Mtwara
Mikindani.
Baadhi ya Abiria walioshuka katika Basi Hilo wakishuhudia jitihada za kuudhibiti moto huo uliotaka kuteketeza basi hilo