Home »
Uncategories »
ZIARA YA ZITTO KABWE KANDA YA MAGHARIBI, JIMBO LA IGALULA
ZIARA YA ZITTO KABWE KANDA YA MAGHARIBI, JIMBO LA IGALULA
Unknown
1:52 PM
Siku ya 5 ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetufikisha Jimbo
la Igalula, wilaya ya Uyui. Tumekutana na wananchi katika vijiji vya
Goweko, Loya, Miswaki, Miyenze na Kigwa.
Tumezungumza kuhusu changamoto ya usafiri wa Reli, wafugaji
kunyanyaswa na watendaji wa kata na askari kwa kunyanganywa mifugo, zao
la Tumbaku, maji safi na salama na suala la jumla la Katiba na mchakato
wa kuandika katiba.
Kimsingi shughuli za kiuchumi za wananchi ni kubwa na hasa Kilimo na
mifugo. Hata hivyo ukosefu wa miundombinu unafanya wananchi wasipate
thamani ya mazao yao na jasho la kazi zao.
Nilipofika Kijiji cha Loya nimeona eneo kubwa lina miti ya mihama.
Wananchi wanatumia tu mihama wakati wa njaa na mara nyingi matunda
haya yanaharibika tu. Lazima matunda haya yana matumizi yake ya
kiviwanda maana ‘kernel’ yake ina mafuta.
Na hili ni swali aliloacha Mh Zitto Kabwe Nani anajua matumizi ya Mihama?