Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akifunguka.
Akiwa amezungukwa na jopo la wahariri wa Magazeti Pendwa ya Global
Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar hivi karibuni, kwa utulivu wa hali ya
juu, Steve Nyerere alifunguka mengi.
Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Katika intavyu hiyo, maswali yaliulizwa kwa mtindo wa kupokezana na
umakini wa hali ya juu ambapo ‘komediani’ huyo aliweka bayana jinsi
ambavyo wasanii wamekuwa wakibadilishana wapenzi kama siti za daladala
huku ugomvi, majungu na unafiki vikichochewa na tabia hiyo.Bila kuonesha woga wala wasiwasi, mwenyekiti huyo alikiri kuwa wasanii wengi wenye majina makubwa ndani na nje ya Bongo Muvi, ndiyo vinara na wafuasi wakubwa wa mtandao huo mchafu wa ngono.
Aliongeza kuwa, ilifika wakati klabu hiyo ikawa inatafsiriwa kama uwanja wa kugawana wapenzi kama mbegu za mahindi.
AWATAJA VINARA
MIGONGANO
Alisema kuwa wapo ambao kwa namna moja au nyingine wamesababisha migogoro na migongano mikubwa ndani ya klabu hiyo kufuatia vitendo hivyo vya kuchangia wapenzi kama wafanyavyo wanyama ndani ya mbuga za Serengeti, Mikumi na nyinginezo.
“Ni kweli kabisa vitendo vya ngono, kubadilishana na kuchangia wapenzi vimekithiri Bongo Muvi.
Wema Sepetu.
“Utakuta msanii huyu wa kiume anatoka kimapenzi na msanii yule wa
kike, lakini wasanii wengine nao bado watataka kumchukua mmoja wao. Au
msanii yuko katika uhusiano na msanii mwenzake, lakini anaanzisha
uhusiano na mwingine bila kujali kuwa huyo naye ana mwingine na anamjua.“Mzunguko unakuwa mkubwa na wanaoongoza kwa ufuska huo ni hawa wasanii ambao wanaonekana mastaa.
Miriam Jolwa 'Kabula'
MFANO“Kwa mfano, wasanii kama (akawataja majina) walikuwa na ‘cheni’ hii ya wapenzi, ...(akamtaja jina) alikuwa na uhusiano na ...(akimtaja shori mkali wa sinema za Kibongo), wakati huohuo,... (akamtaja staa mwingine jina) ana uhusino na msanii ambaye alikuwa kuwa na.... (akawataja kwa majina), sasa unaona jinsi ambavyo mzunguko unakuwa wa hatari zaidi,” alisema Steve Nyerere.
Blandina Chagula ' Johari'
AMELALA NA WANGAPI?Bila kutegemea, msanii huyo aliulizwa na kutakiwa ataje wasanii ambao aliwahi ‘kudondoka nao kunako sita kwa sita’ ambapo alishikilia msimamo kuwa hajawahi kwa sababu ambazo alizitaja kwa hisia kali.
Vicent Kigosi ' Ray'.
Jamaa huyo aliweka angalizo kuwa si rahisi kwa mtu kuamini kuwa yeye
hajawahi kucheza mchezo wa ‘baba na mama’ na msanii yeyote ndani ya
kundi hilo.KIBAO CHAMGEUKIA
Swali: Vipi skendo ya wewe kuwakuwadia wasanii wa kike kwa vigogo?
Steve: (akikunja ndita) hapana jamani, hayo ni maneno tu, mwanzoni watu wengi walidhani hivyo, lakini mimi niliwavuta vigogo ndani ya klabu kwa lengo la hisani na udhamini, namshukuru Mungu baadaye walinielewa, lakini vigogo wote walijitoa kwa sababu ya maneno kama hayo.
Swali: Bifu lako na Ray (Vincent Kigosi) na JB (Jacob Steven) lilikuwaje?
Steve: Ni mambo ya kazi tu, si unajua binadamu tuna mapungufu, tulijikuta katika tofauti za kibinadamu, lakini kwa sasa mambo yako sawa.
Swali: Vipi madai ya kwamba una ‘ngoma’?
Steve: (akitabasamu) jamani, mimi nimepitia misukosuko mingi, lakini nimeendelea kushikilia nafasi yangu ya usanii. Ni kweli walizusha lakini ukweli ukabaki kuwa niko salama.
“Lakini si jambo geni kwa mtu kuzushiwa ugonjwa huo, hata ninyi (wahiriri) mnaweza kusingiziwa mambo mengi na maadui wenu kwa hiyo ni uzushi, niko fiti na tayari kwa mapambano.”
Swali: Eti wewe ni mtu wa ushirikina sana?
Steve: Duh! Si kweli jamani, nimezaliwa na kukulia kwenye familia ya Kikristo, namwamini Mungu kuliko kitu kingine chochote, siwezi kufanya hivyo.
Swali: Ilidaiwa ulimuua mwanao kwa kumtoa kafara, hili likoje?
Steve: (utulivu kidogo, anakuna kichwa) hakuna kitu kama hicho, kama nilivyosema hapo awali mimi ni Mkristo, mambo ya riziki hupangwa na Mungu, sasa nimtoe mwanangu kafara kweli? Siwezi jamani, siyo kweli.
Jacob Steven"JB'.