STAA wa sinema za Kibongo, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufundishwa mila za kimasai na kusema ameelewa, muda mchache baadaye akachemka.
Chuchu Hans (kushoto)katika pozi.
Tukio hilo lililogeuka kituko, lilitokea hivi karibuni ambapo Chuchu
akiwa na wasanii wenzake walifika katika Kijiji cha Misherani kilichopo
mkoani Arusha kwenda kurekodi sinema lakini alivutiwa na mavazi ya
kimasai ndipo alipoomba kujifunza mila za kabila hilo.“Daah! Niliabika maana mbaya zaidi nilielekezwa na binti mdogo nikamwambia tayari nimeweza lakini nilipokwenda kuvaa, nikavaa ndivyo sivyo, acha nichekwe,” alisema Chuchu.
Chuchu Hans (wa poli kutoka kulia) na watoto wa Kimasai.
Hata hivyo, baada ya kukosea huko, Chuchu alisema alijifunza upya na
kuhakikisha kuwa ameweza hivyo kufuta aibu ya awali huku akiwasisitiza
wasanii wenzake kujifunza mila tofautitofauti.