Ndugu yake Peter alifunga ndoa mwaka jana mwezi wa 11 na
harusi yake ilikuwa na watu kama Don Jazzy,Genevieve Nnaji,May D,Emanuel
Adebayor,Diamond na wengine.
Baada ya miezi mitatu hivi sasa ni zamu ya Paul Okoye ambaye anatarajia kufunga
ndoa mwezi wa tatu na mchumba wake Anita Isama.
Msemaji wa P Square amesema Paul na Anita wamechagua tarehe hiyo na kuamua
kuiweka wazi kwa marafiki na mashabiki wao.
Wawili hawa tayari wana mtoto wa kiume na wamekaa muda mrefu kwenye uhusiano
wao hadi hivi sasa kuamua kufunga ndoa.