Picha hii haihusiki na ajali ya basi la Zuberi iliyotokea mchana huu huko wilayani Ikungi.
Mwandishi wetu, Ikungi
BASI
la Zuberi lenye namba T119 AA2 limepata ajali mbaya katika kijiji cha
Nkuhi wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida na watu wanne wameripotiwa kufa
papo hapo kwa kukatwa vichwa huku majeruhi wengi wakiwa wameumia vibaya
sehemu mbalimbali za mwili.
Akizungumza
na MOblog kutoka eneo la tukio leo mchana huu, mwandishi wa habari,
Nathanieli Limu amesema basi hilo la Zuberi lilikuwa linatoka Mwanza
kuja Dar na lilikuwa na zaidi ya abiria 60.
Amesema
kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa basi hilo alikuwa anajaribu kumkwepa
bibi kizee aliyekuwa anakatisha barabarani kwenye majira ya saa saba
mchana.
“ilikuwa
si ajali ya kawaida baada ya bibi kizee kukatiza barabarani na wakati
dereva anajaribu kumkwepa alirudi mara ya pili barabarani ndipo hapo
gari lilipinduka na kuanguka kwenye mtaro,” amesema Limu
Alilisitiza
kwamba mashuhuda wa ajali hiyo wanahusisha tukio hilo na imani za
kishirikiana baada ya bibi huyo kuamua kurudi mara ya pili barabarani na
kusababisha ajali na kukaa kwa muda mrefu eneo la tukio.
Amesema
kwa basi hilo la Zuberi liliinuliwa na lori lenye kifaa maalumu cha
winch baada ya basi hilo kumlalia mtoto mdogo wa miezi kadhaa ambaye
mama yake ni miongoni mwa waliofariki dunia papo hapo na maiti yake
kupelekwa hospitali ya mkoa wa Singida.