MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayeunda kundi la Makomandoo Fredy Wayne ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na Jacqueline Wolper amesema ameachana naye na sasa yupo na nyota mwingine wa filamu, Kajala Masanja. Akizungumza FC hivi karibuni, Fredy alisema msanii huyo amemchanganya mno kimapenzi kiasi kwamba ameamua kumwandikia wimbo unaitwa Ushaniroga, kuonyesha ni jinsi gani amedata naye.
“Siyo siri jamani ndiyo kashaniroga, nampenda na yeye kaonyesha upendo wake kwangu, nipo naye na kuhusu huyo Jack Wolper ni maisha tu, ni rafiki zangu, huwa naona nao katika maeneo tunapiga kiss, ni vitu vya kawaida lakini sasa niko na Kajala,” alisema.
Hata hivyo, wadada hao wawili wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo hawakuweza kupatikana ili kuzungumzia habari hiyo ambayo ni gumzo ya jiji kwa sasa.
filamucentral
filamucentral