BREAKING NEWS:. VURUGU KUBWA ZATOKEA NA KUZUA MTAFARUKU MSIKITINI JIJINI MOMBASA NCHINI KENYA

 Askari akijihami wakati wa vurugu kubwa zilizozuka leo majira ya jioni Jiji la Mombasa wakati Waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti 'Masjid Mussa' ambapo waumini hao wamedaiwa kuwa walikuwa wameandaa mkutano wa hadhara waliouita Kongamano ambalo Serikali ilikataa kuwepo kwa muhadhara huo na wao kupinga maamuzi hayo. 
 Imeelezwa kuwa Baada ya kukatazwa kufanya muhadhara huo, waliamua kuweka Bendera ya Kiislamu katika Msikiti huo huku wakitoa 'Fatwa' kuwa kuanzia leo hawaitambui Bendera ya Kenya, jambo ambalo lilipelekea kutokea kwa vurugu hizo baina ya Askari na waumini hao. Aidha imeripotiwa kuwa watu kadhaa wamefariki dunia katika vurugu hizo na wengine kujeruhiwa.

 Polisi wakiwadhibiti waumini wa dini ya kiislamu jijini Mombasa, nchini Kenya
Mmoja kati ya waumini hao akiwa hoi baada ya kujeruhiwa katika vurugu hizo.
Mmoja wa majeruhi


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...