Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania Luis Aragones amefariki
dunia, akiwa na miaka 75, jumamosi ya leo katika clinic moja jijini
Madrid, daktari Pedro Guillen amethibitisha.
Kocha huyu atakumbukwa kwa kuiongoza Hispania katika awamu mpya ya
mafanikio mnamo mwaka 2008, alipoiwezesha timu hiyo kutwaa kombe la EURO
na baada ya hapo alistaafu na kumpisha Del Bosque. Aliifundisha Spain
kuanzia mwaka 2004 - 2008.