Na Somoe Ng'itu, Dar es Salaam
KATIKA
kuhakikisha Yanga inasonga mbele katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa
wa Afrika kwa kuwatoa mabingwa wa zamani wa michuano hiyo barani Afrika,
timu ya Al Ahly ya Misri jumla ya Sh. milioni 200 zimechangwa
imefahamika.
Habari
kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo ya jijini Dar es Salaam zinasema
kwamba kiasi hicho cha fedha kimechangwa na viongozi wa tano wa mabingwa
hao watetezi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara inayoendelea hapa
nchini.
Chanzo
hicho kiliwataja baadhi ya viongozi hao wa Yanga waliofanikisha fedha
hizo zinapatikana ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Seif
Ahmed 'Magari', Mwenyejiti wa Kamati ya Usajili, Abdallah Binkleb na
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga na Kamati ya Mashindano, Mussa
Katabaro.
Mjumbe
mwingine ambaye yuko katika kamati hiyo maalumu ya kuisambaratisha Al
Ahly ni Isack Chanje na waliamua kuandaa fedha kwa sababu wanajua
zitawasaidia kufanya kila jambo linalowezekana ili kufanikisha malengo
yao.
Chanzo
hicho kiliongeza kwamba klabu ya Yanga imejipanga kuhakikisha mwaka huu
inaweka rekodi ya kumuwaondoa Waarabu katika mashindano hayo na kusonga
mbele.
Aliongeza
kuwa wanafahamu mechi hizo mbili ( nyumbani na ugenini) zitakuwa ngumu
na wapinzani wao wamejipanga kusaka ushindi ili wasonge mbele.
"Tunajua
ni mechi itakayokuwa na ushindani na changamoto mbalimbali, tunataka
kuweka historia na tunajua wazi tukishinda, dunia nzima itajua na
tutasimama kifua mbele," alisema mmoja wadau hao wa Yanga.
Alieleza
kuwa Yanga imejipanga kuhakikisha inapata matokeo mazuri hapa nyumbani
ili mechi yao ya marudiano itakayofanyika Cairo iwe nyepesi.
"Kila
mtu anatakiwa kupata ushindi usio na mashaka nyumbani ili ugenini
unaenda kumalizia, tunawajua waarabu wanavyokuwa ugenini na
wanavyobadilika nyumbani kwao, kikubwa tunataka kufanya kila
kinachowezekana ili tusonge mbele," aliongeza.
Alisema
wakati wanapambana kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, pia
wanahakikisha wanashinda mechi za ligi ili waweze kutetea ubingwa wao.
Wawakilishi
hao wa Tanzania watacheza mechi za hatua ya kwanza baada ya kuwapa
kichapo cha aibu timu ya Komorozine ya Comoro cha mabao 12-2.
Yanga
pia baadaye mwaka huu itaiwakilisha Tanzania Bara katika mashindano ya
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
mwisho.
(Habari hizi zimeandikwa na Somoe Ng’itu wa gazeti la NIPASHE)
Mwarabu lazima afe; Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa ya Yanga SC, Seif Ahmed 'Magari' katikati akiwa na Makamu wake, Mussa Katabaro kushoto |