OMAR Changa, straika aliyekuwa na umbo
la mwili lililokuwa likiendana na nafasi yake hatunaye, na habari kutoka
kwa ndugu zake zinasema alinyongwa na watu wasiojulikana pamoja na
kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya kichwani na ubavuni.
Mchezaji huyo aliyetamba na Yanga
alizikwa jana jioni katika makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Dar
es Salaam huku kifo chake kikiacha maswali mengi ya utata kuliko
majibu.
Kwa mujibu wa kaka wa Changa, ambaye
alikuwa mchezaji wa Moro United iliyoshuka daraja, kaka wa marehemu Idd
Kambi, ameliambiaa Mwanaspoti kuwa kwa mujibu wa ripoti ya daktari
aliyokabidhiwa baba wa marehemu, inaonyesha kuwa Omar Changa alichomwa
na kitu chenye ncha kali mgongoni na kilichotokeza mbele ye tumbo huku
pia shingo ikionekana kulegea.
“Mpaka sasa tumemaliza mazishi, lakini
bado tuna huzuni kuhusu hii ripoti tuliyopewa, tunachofanya tunafuatilia
ni timu gani aliichezea mara ya mwisho kwa sababu inaonekana inafichwa,
lengo ni kujua mazingira ya mchezo yalikuwaje.”
Mdogo huyo wa marehemu alisema Omar
Changa alimpigia simu Jumamosi iliyopita, akimtaka kwenda naye
kushuhudia anavyocheza ndondo mchangani maeneo ya Kigamboni nje kidogo
ya jiji la Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Changa alifunga bao moja la ushindi kwa penalti.
Mchumba wake marehemu aliyetambulika kwa
jina la Sarah Mahemba alisema Changa hakurudi kwake tangu alipoondoka
Jumamosi kuelekea Kigamboni katika mchezo huo, jambo ambalo liliwapa
shaka wapangaji wenzake siku ya Jumapili na kuamua kumtafuta kupitia
simu yake ya mkononi lakini haikupatikana ingawa yeye aliijaribu na kuwa
inaita bila kupokelewa mpaka alipopata taarifa za kifo kupitia mdogo wa
mshambuliaji wa Mbeya City, Omari Kijuso.
Mwili wa marehemu ulipatikana katika mtaro, maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)