Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Askari
polisi watano mkoani dodoma wamefariki dunia papohapo katika ajali ya
gari iliyotokea 31/01/2014 majira ya saa 5 usiku katika barabara
kuu ya Dodoma – Morogoro eneo la Mtumba Center, Kata ya Mtumba Tarafa ya
Kikombo Manispaa ya Dodoma, ambapo gari namba ya usajili T.770 ABT Toyota Corolla
lililokuwa likiendeshwa na Askari mwenye namba H. 3783 PC DEOGRATIUS wa
Wilaya ya Kongwa.Gari hilo lilikuwa likitokea Dodoma mjini likielekea Wilayani Kongwa
liligongana uso kwa uso na gari namba T.997AVW Scania Bus mali ya
Kampuni ya Mohamed Trans lililokuwa likiendeshwa na JUMA s/o MOHAMED,
miaka 38, Mkazi wa Mwanza, likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma na
kusababisha vifo kwa askari watano papohapo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME amewataja Askari hao waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni:-
1. D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye miaka 51, Mgogo.
2. F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye miaka 34, Muha.
3. H.3783 PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
4. WP.10337 PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
5. WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye miaka 20, Mhehe.
Wote ni askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.
Kamanda
MISIME amesema chanzo cha ajali hiyo kulingana na uchunguzi wa awali ni
mwendo kasi kutokana na uharibifu uliotokea kwa gari dogo walilokuwa
wamepanda askari na jinsi lilivyoburuzwa na basi kwa umbali wa mita 56
kisha kwenda kusimama umbali wa mita 97, kwa hali hiyo umbali kutoka
eneo walipogongana hadi basi liliipoenda kusimama ni mita 152. Dereva wa
Bus alitoroka mara baada ya ajali hiyo kutokea, juhudi za kumtafuta
zinaendelea. Miili ya marehemu imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali
ya mkoa Dodoma.