MADEREVA wote wa daladala Manispaa ya Morogoro leo wamegoma kutoa huduma ya usafiri wakilalamikia kukamatwa hovyo na maafande wa Kikosi cha Usalama Barabarani katika manispaa hiyo.
Akizungumza na tovuti hii, mmoja wa madereva wa daladala hizo, Bw. Ramadhani Shukuru alisema kwamba kwa siku gari linakamatwa mara mbili na kwamba ukifikishwa kituoni unalipishwa faini ya shilingi 90,000/=
"Unakamatwa asubuhi unalipa 90,000/= makosa matatu, ukiachiwa na kuanza kazi ukifika Kihonda unakamatwa tena ukijitetea askari anakwambiaa yeye hausiki na kukamatwa kwako kwani amekukamata kwa makosa mengine unaenda tena kituoni wanakukamua 90,000/= nyingine kesho unakamatwa tena, sasa si bora tuegeshe magari tukalime matombo!" alisema Rama.
(PICHA ZOTE NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)