Kamanda
wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar akiongoza Operesheni wa kukagua
magunia yaliyokuwa na Pembe za Ndovu yaliokamatwa katika bandari hiyo
leo yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya nchi kupitia bandari
hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari Kikosi cha
KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40. Magunia
haya yakiwa na shehena na makombe ya Pwani wakati katikati yakiwa na
viroba vya Pembe za Ndovu ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika Kontena
likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, limegunduliwa katika bandari ya
Zanzibar leo asubuhi. Baadhi
ya Pembe za Ndovu zilizokamatwa katika bandari ya Malindi Zanzibar
yakisubiri kuhesabiwa kupata idadi kamili, thamani yake na uzito kwa
ujumla. Operesheni ya kuhesabu Pembe za Ndovu zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar ikiendelea.