Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Absalom Bohella (Kuliai) akizungumza na Timu ya Ukaguzi
wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ilimpotembelea Ofisini kwake kukagua kukagua mirdai ya maendeleo Bandari
hapo. Kutoka kushoto ni viongozi wa Timu hiyo, Prof. Longinus
Rutasitara (Wakwanza Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Katikati).
Afisa
Miradi Mwandamizi wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kalebwe (Kushoto)
akitoa maelezo ya uendelezaji wa maeneo ya Bandari hiyo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara Bandarini hapo.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais ikijionea eneo la Bandari ya Mtwara ambapo panapotarajiwa kuongezwa magati
Afisa
Miradi Mwandamizi wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kalebwe (Wambele
Kushoto) akiwaonesha Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango eneo jipya (halionekani) ambalo Bandari hiyo
imeliongeza ili kuboresha ufanisi bandarini hapo.
Shehena ya korosho ikiendelea kupakiwa katika makontena tayari kusafirishwa.
Afisa
Miradi Mwandamizi wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kalebwe (Wambele
Kushoto) akiwaonesha Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango eneo jipya (halionekani) ambalo Bandari hiyo
imeliongeza ili kuboresha ufanisi bandarini hapo.
Picha na Saidi Mkabakuli
Ujenzi wa eneo la kuhifadhia saruji ukiendelea
Na Saidi Mkabakuli
Mamlaka
ya Bandari Tanzania, kupitia Bandari yake ya Mtwara inajidhatiti katika
kuiboresha ili kuiongezea uwezo wa kuhudumia mizigo iingiayo na itokayo
mkoani humo kupitia bandari hiyo kufuatia kuongezeka kwa shughuli za
biashara mkoani Mtwara.
Akizungumza na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Absalom Bohella amesema kwamba hatua
hii inachagizwa na mkakati wa kukabiliana na kasi ya maendeleo ya
ukuaji wa uwekezaji katika maeneo ya viwanda vikubwa na biashara za
huduma mkoani Mtwara.
Aliongeza
kuwa mkakati huu unajumuisha upanuzi wa eneo la bandari hiyo kutoka
hekta 70 zilizokuwa zikimilikiwa na Bandari tangu kuanzishwa kwake mwaka
1950 hadi kufikia hekta zaidi ya 2600 pamoja na upanuzi wa magati manne
ya kuhudumia meli bandari hapo.
“Upanuzi
huu utaongeza kasi yetu ya kuhudumia mizigo toka tani za ujazo 270 za
sasa hadi kufikia tani za ujazo 400 kwa mwaka hii itatuongezea ufanisi
katika kuhudumia watumiaji wa Bandari yetu, hasa kufuatia kugundulika
kwa gesi mkoani Mtwara,” alisema Bw. Bohella.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi
Florence Mwanri ambaye ni mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa
miradi hiyo alisema kuwa kuna haja ya dhati ya kuwekeza katika Bandari
hiyo ili kukabiliana na kasi ya maendeleo ya mkoa wa Mtwara kufuatia
wawekezaji wengi kuendelea kumiminika na kuchangamkia fursa za uwekezaji
zilizomo mkoani humo.
“Bandari
ya Mtwara ina fursa za nyingi za kuhudumia wafanyabiashara wa ndani na
nje ya nchi, hasa katika kipindi hiki cha uchumi wa gesi mkoani Mtwara,
hivyo uendelezaji wa upanuzi wa bandari hii ni suala la kimkakati,”
alisema Bibi Mwanri.
Kwa
mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 -
2015/16), Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa
katika miundombinu ya nishati, usafirishaji (bandari, reli, barabara na
usafiri wa anga), maji (safi, taka na ya uzalishaji) na TEHAMA.
Serikali
imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa
kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni
kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji
mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi. Mpango wa Kwanza
wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango
mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na
kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi
ya maendeleo kitaifa.
Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.