Meneja
Huduma Maji taka kutoka Dawasco, Mathias Mulagwande (mwenye suti ya
damu ya mzee) akinyoosha kidole kumuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Meck Sadick (wa pili kulia) sehemu korofi za kutiririsha
maji machafu barabara ya Morogoro kati kati ya jiji.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
WATENDAJI wa Mamlaka za Maji
Safi na Taka, Manispaa, Halmashauri, Wakala wa Barabara na Mabasi
yaendayo kasi wameshauri kuwa na utaratibu wa kuwasiliana na
kushirikiana kwa pamoja ili kuleta tija katika usombaji taka katika jiji
la Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wetu,
kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Said Meck Sadick,
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark
Shayo amesema kuwa tatizo la jiji la Dar es Salaam ni watendaji wa mkoa
hawana mawasiliano ya kutosha katika utendaji kazi wa kila siku.
Shayo alizungumza hayo kwenye
ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya kugagua hali ya usafi
katika maeneo kadhaa pamoja na kuangalia maeneo korofi katika
kutitirisha maji machafu kwenye mitaro kadhaa kati kati ya jiji.
“tatizo kubwa katika jiji la Dar
es Salaam ni watendaji wa jiji, manispaa, wakala wa barabara, Tanesco
na mamlaka za maji safi na taka kutokuwa na utaratibu wa kuwasiliana
katika utendaji kazi wa kila siku katika kuboresha usombaji wa taka
kwenye jiji la Dar,” amesema Shayo
Meneja Huduma Maji taka kutoka
Dawasco, Mathias Mulagwande akiwaonyesha baadhi ya viongozi wa Mkoa wa
Dar es Salaam, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick na Mbunge
wa Ilala, Mussa Zungu baadhi ya mashimo (Potholes) ambayo ni hatari kwa
wananchi watembea kwa miguu baada ya ujenzi wa barabara ya mabasi
yaendayo kasi.
Shayo alilisisitiza kwamba
katika utendaji kazi wa jiji kama la Dar inahitajika ushirikiano wa
dhati kati ya wadau wa kusomba taka na watendaji wa manispaa pamoja na
jiji ili kuweka mkoa wa Dar es Salaam katika hali safi wakati wote.
Amesema kuwa ingawaje tatizo
kubwa la uchafu linasababishwa na miundombinu mibovu ya barabara na maji
hasa kuelekea katika dampo kuu la mkoa sehemu ya Pugu Kinyamwezi,
Gongo la Mboto.
Shayo ambaye kampuni yake
inajishughulisha na usombaji wa taka ngumu na nyepesi katika mkoa wa Dar
es Salaam amesema kwamba mamlaka zinazohusika kwa kushirikiana na wadau
lazima watoe elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi
taka.
“sehemu ya dampo la Pugu
Kinyamwezi. inahitajika kampuni ya ujenzi yenye uwezo wa kuboresha
miundombinu ya barabara kuelekea kwenye dampo ili kupunguza foleni ya
magari ya taka na kuongeza tija ya kazi katika eneo husika,” aliongeza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh
Said Meck Sadick akiongoza msafara wa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Dar
es Salaam katika kuangalia hali ya usafi na miundombinu ya maji na
barabara jijini Dar.
Kwa upande wake, Minael Mshanga
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, amesema jiji limejipanga kufanya ukarabati wa
miundombinu ya barabara kuelekea dampo ili kuongeza kasi ya magari
yanayokwenda kumwaga taka katika dampo hilo.
“hivi tupo katika hatua za
mwisho na tumempata mkandarasi wa kuja kujenga na kutengeneza
miundombinu ya barabara kuelekea katika dampo pamoja na kutengeneza
mataa katika eneo husika ili kazi ya kutupa taka ifanyike usiku na
mchana,” amesema Mshanga
Aliongeza kwamba jiji lina
mpango wa kuanza kushirikiana kwa karibu na wakandarasi wazalendo katika
kuleta ufanisi wa usombaji taka ili kuzuia magonjwa ya mlipuko katika
mkoa wa Dar es Salaam.
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu
akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick wakati wa
ziara ya ghafla ya kugagua hali ya miundombinu ya maji na barabara kati
kati ya jiji la Dar.
Baadhi ya magari ya wakazi wa
jiji yakipita kwa taabu katika madimbwi na mashimo ya maji machafu kati
kati ya jiji la Dar es Salaam.
Viongozi
wa mkoa wa Dar es Salaam wakijadili moja ya sehemu korofi kati kati ya
jiji karibu na Haidery Plaza ambapo kipindi cha mvua maji taka
yaliyochanganyikana na kinyesi yanatuama kwa kipindi kirefu ambapo
hakuna mfereji wala mtaro wa maji machafu.
Mashimo ya miaka nenda rudi yasiyopatiwa ufumbuzi lakini baada ya ziara yatarekebishwa.
Mkuu wa mkoa wa Dar, Said Meck Sadick akitoa ushauri kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Jackson Midala (mwenye tai nyeusi).
Kaimu Mkuu wa Idara ya Udhibiti
taka kutoka jiji, Enezael Ayo (kushoto) akifafanua jinsi magari ya taka
yanavyomwaga taka katika dampo kuu la Pugu Kinyamwezi jijini Dar wakati
wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Dar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tirima
Enterprises, Robert Ngeleshi akizungumza changamoto na matatizo ya
mawakala wa kusomba taka katika jiji la Dar ambao waliongozana na Mkuu
wa mkoa kwenye ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akielezea jambo kwa mkuu wa
mkoa wakati wa kuhitimisha ziara hiyo katika maeneo ya dampo Pugu
Kinyamwezi.
Moja ya Bull dozer linalorekebisha barabara likiwa limeharibika kutokana na miundombinu mibovu katika dampo la Pugu Kinyamwezi.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Minael
Mshanga (kulia kwa Mkuu wa Mkoa) akitoa ufafanuzi wa matatizo na
changamoto za usombaji na utupaji taka katika dampo la Pugu Kinyamwezi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck
Sadick akiagana na wakandarasi wa usombaji taka na watendaji wa jiji.
Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.