Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiwa katika daraja la Chimate ambalo mbao zake zimeoza na kupelekea kuhatarisha usalama wa watumiaji wa Daraja hilo katika Wilaya ya Nyasa. Ametoa agizo kwa Meneja wa TANROADS mkoani humo kubadili mbao katika daraja la Mto CHIMATE haraka na kuweka kambi katika daraja la Mto MBULI kufanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na wananchi ili kujua tabia ya mto huo hasa wakati wa masika.
Kutokana na Mvua kubwa zinazoelendelea kunyesha Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma zimesababisha madhara makubwa katika vijiji viwili ndani ya wilaya hiyo ikiwemo kuharibu mazao mashambani pamoja na kusombwa kwa daraja la mto Mbuli katika kijiji cha Ng’ombo.Hali hii imepelekea wakazi hao kupata tabu pale wanapougua huku wanafunzi wakishindwa kwenda shule kwa muda wa mwezi mmoja na wengine mashamba yao kusombwa na maji.
Hali hiyo
imepelekea huduma za kijamii kuwa ngumu kufanyika ikiwa ni pamoja na
upande wa matibabu pamoja na mahudhurio ya watoto shule.
Pichani aliyesimama katikati ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwangu akiwa katika Daraja la kijiji cha
MBUI ambacho daraja la mto ng’ombo limesombwa na maji na
kukigawa kijiji hicho sehemu mbili, sehemu moja ikiwa inashule na
sehemu moja kukiwa na zahatari.
Pichani ni dereva wa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma aliyejulikana kwa jina moja la Komba akitoa msaada wa kuwavusha watoto wa shule katika daraja la mto Mbuli ambalo nilamuda lililotengenezwa na wananchi wenyewe wa kijiji cha Ng’ombo.
Kulia ni mwenyekiti wa CCM Mh.Oddo Mwisho akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kuhusiana na Daraja hilo lilisombwa na maji.
Pichani ni wakazi wa Kijiji cha Ng'ombo wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ambaye hayupo pichani akiwataka wakazi ho kuwa na subila katika ujenzi wa daraja hilo kutokana na Mto huo kuwa na tabia za kuhamahama. Hivyo akatoa agizo kwa wataalamu kuja na kuweka kambi ili kujua namna ya kuweza kuudhibiti mto huo usijeukasababisha maafa tena katika ujenzi huo pale utakapotengamaa.
Katika picha ni wakazi wa kijiji cha Ng'ombo wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma ambaye hayupo katika picha huku wakiwa katika nyuso za majonzi kutokana na mvua kusababisha uharibifu.(Picha zote na Demashones)