Wachezaji wa Manchester City wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe hicho.
Na Riziki Mashaka.
Timu ya Manchester City imenyakua ubingwa wa kombe la Capital One baada ya kuitandika Sunderland kwa magoli 3-1 katika dimba la Wembley.
Mshambuliaji wa Sunderland, Fabio Borini alipachika goli mnamo dakika ya 10 na kuiandikia timu hiyo goli la pekee, Sunderland ilikuwa kifua mbele kwa goli 1-0 mpaka kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Kiungo wa Man City, Yaya Toure alipopachika goli la kwanza
Mtanange huo ulichukua sura mpya katika kipindi cha pili baada ya kiungo wa Manchester City, Yaya Toure kusawazisha goli hilo mnamo dakika ya 54, wakati mashabiki wa Man City wakishikwa na butwaa baada ya goli hilo, hali ilizidi kupamba moto kwani Samir Nasri alipachika goli la pili mnamo dakika ya 56 na kuifanya timu hiyo kuwa mbele kwa magoli 2-I.
Samir Nasri alipokuwa anashangilia baada ya kupachika goli la pili.
Timu hizo zilikuwa zikishambualiana mara kwa mara, na mpaka kufikia dakika ya 69 mshambuali wa Man City, Sergio Aguero alishindwa kuonesha makali yake na hali hiyo ilipelekea kocha wake Manuel Pellegrini kumtoa na kumuingiza kiungo mshambualiaji, Jesus Navas ambaye aliipachikia timu hiyo goli la tatu mnamo dakika ya 89 ya mchezo.
Kiungo wa Man City, Jesus Navas alipokuwa apaichikia timu yake goli la 3.
Wachezaji wa Sunderland walipokuwa wanatoka uwanjani baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa.
Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa, Man City ilikuwa kifua mbele kwa jumla ya magoli 3-1, kitendo hicho kiliipelekea timu hiyo kuibuka mabingwa wa kikombe hicho cha Capital One, 2014.
Mashabiki wa Man City walipokuwa wanashangilia ushindi wa timu yao.
Picha aliyoituma mchezaji wa Man City, Vincet Kompany katika mtandao wake wa Twitter, ni baada ya kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo.
Kutoka kushoto ni beki na kapteni wa timu hiyo, Vincet Kompany akiwa amebeba kikombe hicho kwa furaha, kulia ni kocha, Manuel Pellegrini naye akiwa amebeba kikombe hicho cha Capital One kwa mara ya kwanza katika historia yake ya soka la Uingereza.