Mafundi
wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika kusafirishia maji kutoka
Mitambo ya Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la kuhifadhia maji
lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa mafundi
hao wameshasambaza mabomba kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya
kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.
Timu ya mafundi ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu wakiwa kazini katika Ofisi ya Mitambo hiyo, mkoani Pwani.
Kaimu
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Deusdedit Rwegasira (Aliyevaa
fulana la mistari) akiwaonesha Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango video ya namna miundombinu ya maji
inavohujumiwa na baadhi wananchi wasiofuata taratibu zilizowekwa za kwa
kujiunganishia maji kiholela.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ikikagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu
ilipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.
Meneja
wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Kushoto) akiwaonesha
Wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango mashine nne mpya zilifungwa na Serikali hivi karibuni
walipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.
Viongozi
wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na
Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto) na
Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Watatu
Kulia) wakionesha eneo la kusafishia maji katika Mtambo wa Ruvu Chini
walipokuwa katika ukaguzi wa mtambo huo. Kushoto ni Mratibu wa ziara
hiyo, Bibi Salome Kingdom.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ikikagua bomba lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa
siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa mitambo ya Ruvu Chini.
Anayewaonesha ni Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel
Makusa (Wapili Kulia).
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ikiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini,
Mhandisi Emmanuel Makusa (Watatu kushoto) kwenye lenye uwezo wa
kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye
ukaguzi wa mitambo ya Ruvu Chini.Picha na Saidi Mkabakuli