Watu watatu wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya kahama mkoani shinyanga kufuatia ajali ya kugongwa na gari iliyokuwa ikiendeshwa na mkuu wakituo cha polisi cha wilaya ya Kahama Elias Haway huku mmoja akiwa ameumia sana sehemu ya mguu.
Ajali hiyo imetokea Jana majira ya 1.30
usiku katika barabara itokayo isaka kuingia kahama mjiniu ambapo Haway
akiendesha gari yake Toyota Rav 4 lenye namba T 798 BSK alimgonga
mwendesha pikipiki.
Watu waliogongwa wametambuliwa kwa majina ya Joseph Malugu (35) mkazi wa
Majeruhi wa awali Joseph Malugu akiwa hospitali ya wilaya ya Kahama baada ya kuumia vibaya mguu wake na sehemu zingine za mwili.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema
Haway alianza kumgonga mwendesha bodaboda Bw. Malugu katika eneo la
Zahanati ya Igalilimi ambapo watu wenye hasira walimzingira wakimtaka
asimame naye akakimbia huku akiwagonga tena waenda kwa mguu wawili.
Msukuma Toroli Fitina Majuto akiwa Hospitalini Hapo
Wamesema Haway akionekana kuwa
amelewa hakutaka kuwatii watu waliyokuwa wakimweleza ndipo alipoondoa
gari lake kwa mwendo kasi na kwenda kumgonga Bw. Majuto katika eneo la
Mkude ambae aliumia sana kwenye sehemu ya tumbo na kusababisha utumbo
kutoka nje.
Mtembea kwa miguu Cosmas Peter akiwa hoi hospitalini
Shuhuda mmoja Mkulo Iddy amesema
eneo hilo pia Haway hakutaka kusimama na aliendelea na mwendo kasi ndipo
alipokwenda kumgonga mtu mwingine wa tatu Bw. Peter katika barabara ya
eneo la Paradise mitaa ya Nyasubi.
MKUU WA KITUO CHA POLISI KAHAMA ELIUS HAWAII
Haway alipohojiwa amekiri kutokea kwa
ajali hiyo huku alisema kuna upotoshaji mkubwa wa taarifa hiyo kwani
yeye ndiye aliyegongwa na mwendesha pikipiki huyo wa kwanza.
Amesema alipotaka kusimama kumwona mtu
huyo aliyegonga, aliona watu wameanza kumzonga naye akamua kukimbia kwa
usalama wake ndipo alipoweza kuwagonga tena wale wengine wawili.
Mganga Mfawidhi wa Hospitari ya
wilaya ya Kahama Dk Joseph Foma amethibitisha kugongwa na gari watu hao
na wamelazwa katika wodi namba moja katika hospital hiyo, huku hali zao
zikiwa mbaya na kwamba wapo katika utaratibu wa kumuhamishia Malugu
katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza.
Credit: Kijukuu Blog