Zitto Kabwe jana amefanya mkutano wa 3 ndani ya Mkoa wa Kigoma,mikutano hii ilianza siku ya Jumamosi kwa sehemu ya Mwandiga mahali alipozaliwa na kukulia,Kasulu ilikua juzi na jana kafanya Kigoma mjini eneo la Mwanga kwenye uwanja wa Community Centre....
Mkutano
ulianza sa 10 kiitifaki ulitanguliwa na viongozi wa Chadema wa
mkoa,kisha Zitto Kabwe kupanda Jukwaani na moja kati ya vitu
alivyovizungumzia ni kuhusu tamko la Dr.Wilbroad Slaa alipokuwa kwenye
mkutano wake wa Kuimarisha chama uliofanyika Igunga Mkoani Tabora....
Dr.Slaa
alizungumzia kuhusu mikutano anayoifanya Zitto Kabwe kuwa si halali
yeye anatakiwa kufanya kwenye jimbo lake tu ambalo ni Kigoma Kaskazini .
Hiki ndicho alichokizungumza kufuatia tamko hilo la Dr.Slaa "Sasa jana (juzi ) Katibu Mkuu kasema Kwanini nafanya ziara zaidi ya Kigoma Kaskazini siruhusiwi kwenda sehemu nyingine yoyote baada ya kusikia yale mapokezi ya Kasulu.
Hiki ndicho alichokizungumza kufuatia tamko hilo la Dr.Slaa "Sasa jana (juzi ) Katibu Mkuu kasema Kwanini nafanya ziara zaidi ya Kigoma Kaskazini siruhusiwi kwenda sehemu nyingine yoyote baada ya kusikia yale mapokezi ya Kasulu.
"Mimi
nawaambia katiba ya Nchi hii inaniruhusu kwenda mahali kokote,sehemu
yoyote nchi hii kwa mujibu wa katiba maana mimi bado ni Mbunge.Kama
wamenifukuza waseme kuwa wamenifukuza lakini kama hawajanifukuza mimi
bado mbunge"
"Kwa
hiyo nitaenda Kigoma Kaskazini,nitaenda Kigoma Kusini,nitaenda
Kasulu,nitaenda Kigoma Mjini kuhutubia Wananchi na siyo hivyo tu
nitaenda Mpanda,nitaenda Tabora,nitaenda Shinyanga,nitaenda Mwanza
nitaenda hadi Arusha na hakuna mtu wa kunizuia."
Add caption |