Kutoka
kushoto ni Kipaji kipya ndani ya Skylight Band anafahamika kama DONODE,
DIGNA MBEPERA, SAM MAPENZI na ANETH KUSHABA AK47 wakitoa burudani kwa
mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye uwanja wao wa
nyumbani ambapo X-MASS pamoja na BOXING DAY watakinukisha kwenye kiota
cha Escape One kwenye upepo mwanana wa bahari.....Njoo ufurahie
mapumziko yako na Band nambari moja mujini wengine wanafuata.
Aneth Kushaba AK47 katika hisia kali.
Digna Mbepera akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Shabiki
wa Skylight Band Zulekha alishehereke siku yake ya kuzaliwa ndani ya
Thai Village na kupata bahati ya kuimbiwa wimbo maalum wa Happy Birthday
na Divas wa Skylight Band.
Eeeeh Shosti njoo niku-hug mweeee hongera jamani.....!!! Full mashamsham na mashosti zake.
Mashamsham
moto moto....raha iliyoje....!!! Kwa wale wote watakaozaliwa tarehe 25
sikukuu ya X-MASS watapata wasaa wa kuimbiwa wimbo wa Birthday na
Skylight Band kama ilivyokuwa kwa mdau pichani.
Anafahamika
kwa jina la Donode ni kipaji kipya cha Skylight Band.....Lione Richie
wa Bongo njoo umshuhudie X-Mass hii pamoja na Boxing Day ndani ya Escape
One Mikocheni jijini Dar.
Mdogo mdogo mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga kwenye dancing floor Juma lilipotia.
Skylight Band inagusa rika zote haijalishi....kama inavyoonekana pichani.
Nyomi ya mashabiki wa Skylight Band ikiendelea kumiminika kwa dancing floor.
Madada wakijiachia kwa raha zao....!!!
Mary Lukas na Digna Mbepera wakifanya yao jukwaani.
Tuache sie kwa raha zetu.....Skylight Band ndio mambo yote...!!!
Usipime bwana.....Skylight Band ndio mpango mzima...!!!
Mpiga Drumz wa Skylight Band Idrisa akifanya yake.
Yachuma
minataka mukanda ya chuma.....Mguu wa kushot mbele wa Kulia
nyuma......Mashabiki wa Skylight Band wakichiziki na staili hiyo
inayobamba kwa kasi.
Rappa Joniko Flower akisebeneka vilivyo kuwapa raha mashabiki wake.
Aneth Kushaba AK47 naye hakubaki nyuma ni mambo ya SKELEWU........SKELEEEEE...!!!
Baada
ya wiki ndefu sasa ni muda wa ku-enjoy holiday na burudani ya Skylight
Band......Wadau wakiwa wame-relax huku wakigonga vyombo taratibu.....!!!
Mtangazaji wa Luninga namba moja la Vijana EATV, Adrian Hillary Stepp akishow love na mdogo wake.
Digna Mbepera wa Skylight Band akishow love na shosti wake kipenzi.
Wadau wa Skylight Band wakishow love na Ukodak.
Usione kaloa jasho...hii yote ni Gwaride la Skylight Band, huna haja ya Gym hili ni zoezi tosha.
Mduara ulihusika pia kama kawaida.
Baadhi
ya wanafunzi wa Vyuo mbalimbali kikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam-UDSM, IFM, CBE na vingine kibao walijumuika na Skylight Band
kusheherekea mapumziko ya mwisho wa mwaka.
Walimwagaje radhi kwa raha zao....!!!